Hatimaye sakata la usajili wa kiungo mshambuliaji wa Kiargentina Angel Di Maria limefikia tamati muda mfupi uliopita.
Kupitia akaunti rasmi za mitandao ya kijamii ya vilabu vya Manchester United na PSG imethibitishwa rasmi Di Maria ameuzwa.
Di Maria siku chache zilizopita alifuzu vipimo vya afya alivyofanyiwa huko Qatar, Mjini Doha, nyumbani kwa wamiliki wa klabu hiyo.
Winga huyo anategemewa kutambulishwa rasmi leo jioni huko Paris Ufaransa na atasaini mkataba wa miaka minne kuitumikia PSG.
Di Maria
aliyenunuliwa kwa ada ya uhamisho wa Pound Milioni 59.7, anaripotiwa
kuuzwa kwenda PSG kwa ada ya Pound Mil. 44 mwaka mmoja baada ya kujiunga
na United.
on Thursday, August 6, 2015
Post a Comment