Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ akiwa na Mbongo-Fleva Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’.
Imevuja! Gumzo la ndoa ya staa mwenye jina kubwa Bongo, Jokate Mwegelo
‘Kidoti’ na Mbongo-Fleva Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ inadaiwa kupigwa
zengwe kama ilivyowahi kutokea kwa Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’
kufuatia madai ya mwanadada huyo kumtambulisha jamaa huyo kwao kisha
kukataliwa.
MINONG’ONO
Habari kutoka chanzo cha kuaminika ambacho ni mtu wa karibu wa wawili
hao, tukio hilo lilijiri hivi karibuni ambapo wawili hao walihudhuria
kwenye harusi ya dada wa Jokate hivyo kuibua minong’ono kwamba huenda
harusi inayofuata itakuwa yao.
Chanzo hicho kiliendelea kudai kwamba, habari mbaya ni kuwa baada ya
Jokate kumtambulisha Kiba kwa ndugu, jamaa na marafiki baadaye kumpeleka
kwao, wazazi wa mwanadada huyo walikuja juu wakidai jambo hilo
haliwezekani huku sababu nne zikianikwa.
KIGEZO CHA DINI
Madai yalishushwa kuwa, sababu ya kwanza ni kwamba, familia ya Jokate
hasa wazazi wake ni watu walioshika sana Dini ya Kikristo (Kanisa
Katoliki) huku Kiba akiwa ni Muislam kama ilivyokuwa kwa Diamond
aliyeshindwa kumuoa Jokate kwa kigezo hichohicho.
NDOA ZA MASTAA NI TATIZO?
Ilidaiwa kuwa, sababu ya pili iliyotolewa na wazazi hao ni kwamba, hawataki binti yao kuolewa na msanii mwenzake kwa kuwa wanajua ndoa za mastaa zinavyokuwa na ‘drama’.
Ilidaiwa kuwa, sababu ya pili iliyotolewa na wazazi hao ni kwamba, hawataki binti yao kuolewa na msanii mwenzake kwa kuwa wanajua ndoa za mastaa zinavyokuwa na ‘drama’.
KIGEZO CHA KABILA
Kigezo kingine kilichotajwa ni kabila ambapo wazazi hao wanataka Jokate
aolewe na mtu wa kabila lake la Wangoni tofauti na Kiba ambaye ni Muha.
Mbongo-Fleva Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’.
KIGEZO CHA BONGO FLEVA
Chanzo kilikwenda mbali zaidi na kudai kuwa, wazazi hao wanaamini kwamba baadhi ya wasanii wa Bongo Fleva ni wahuni hivyo kuwawia vigumu kukubali binti yao kuolewa na Mbongo-Fleva.Pia habari za ndani zilidai kwamba, Jokate na Kiba walikuwa kwenye harakati za kuoana kabla ya mwaka huu kumalizika ila zengwe limekuwa kubwa upande wa familia hasa kwenye suala la dini ambapo kila mmoja amekuwa akitaka mwanaye abadili dini.

KAMA DIAMOND
“Unajua kilichompata Kiba ni kama kile kilichomfika Diamond kipindi kile alipotaka kumuoa Jokate.
“Ilikuwa ni ishu hiyohiyo ya dini maana wazazi wa Jokate walikuwa wakimwambia kila siku kama kweli anampenda mtoto wao basi abadili dini lakini Diamond hakuweza kufanya hivyo na kujikuta wakishindwa kufikia lengo la kufunga ndoa,” kilitambaa chanzo hicho.

KIBA KAMA KAWA
Kama kawaida yake, Kiba alipoulizwa juu ya ishu hiyo alikanusha vikali
akidai kwamba hajawahi kuwa na mipango hiyo na mrembo huyo.“Ulishawahi
kunisikia nikizungumzia ishu hiyo? Siyo kweli bwana…hakuna kitu kama
hicho,” alisema Kiba akionekana ‘kumaindi’ kwa kuulizwa juu ya jambo
hilo.Kwa upande wake Jokate hakupatikana hewani na hata alipotumiwa
ujumbe mfupi hakujibu hivyo jitihada za kumpata zinaendelea.
TUJIKUMBUSHE
Kwa muda mrefu, Jokate na Kiba wamekuwa wakiripotiwa kuwa ni wapenzi
lakini Kiba amekuwa mstari wa mbele kukanusha huku Jokate akikiri kuwa
jamaa huyo ni mtu wake.
Post a Comment