Staa
wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ‘Kay’ amefunguka kuwa kutoonekana
kwake kwenye ushabiki wa vyama na wagombea kama wasanii wengine si
kwamba hana ushabiki lakini moyoni mwake yupo Team ya Dk. John Magufuli
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Kajala
amesema kuwa pamoja na mbwembwe za watu kujiweka wazi kuhusu chama na
wagombea wanaowakubali, yeye mambo yake ni kimyakimya kama alivyo
mgombea wake wa urais kupitia chama hicho.
“Nimekuwa
kimya kwa muda mrefu kwa sababu hata mgombea wangu wa urais, Magufuli
ni mtu wa kimyakimya ila mtendaji mzuri, ndiye anastahili kura yangu,” alisema Kajala.
Post a Comment