Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

KAMANDA KOVA AJA KIVINGINE

JESHI  la Polisi  Kanda Maalum ya Dar es Salaam linatarajia kuzindua mashindano ya michezo mbalimbali kwa lengo la kuwashirikisha wananchi  wa  rika zote  na  itikadi  mbalimbali 
yatakayojulikana“KAMISHNA KOVA CUP”.

 Madhumini ya mashindano haya ni  ni  Kuwaunganisha wananchi wenye itikadi mbalimbali ili kupitia mashindano  haya  watakaoshiriki  watajifunza  masuala  ya usalama, uzalendo  na kuzingatia utaifa kwa madhumuni ya kuwashirikisha kikamilifu katika ulinzi wa nchi na kudumisha amani  na  utulivu  katika  jiji  la  Dar  es  Salaam  na  mikoa mingine.

Lengo lingine ni  Kuishirikisha jamii  kuondokana na dhana ya kutenda uhalifu wa aina mbalimbali kama vile ujambazi, matumizi ya aina mbalimbali ya  madawa ya kulevya,  wizi katika mitandao,uzururaji, na kukaa katika vijiwe bila kazi.

Pia  Kupitia michezo mbalimbali, jamii itafaidika kupata elimu juu ya umuhimu wa jukumu la msingi la kushiriki katika ulinzi na usalama  wa  nchi  hii,  itakuwa  ni  fursa  nzuri  kujua madhara ya kujihusisha na vitendo vya uhalifu.

Katika michezo watajifunza kujenga au kuimarisha mahusiano mema baina ya Jeshi la Polisi na  jamii  kwa  ujumla  kupitia  dhana  ya  Polisi  Jamii itatekelezwa kwa vitendo.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top