Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

LOWASSA KUTUA ARUSHA KESHO,MJI KUFUNGWA KWA SAA TANO,SOMA HAPO KUJUA

Mwenyekiti wa Mkoa wa Arusha kupitia chama cha CUF Salussingo Omari
akizungumza na vyombo vya habari.
Waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa ambaye ni mgombea Urais kupitia chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA)anatarajiwa kupokelewa kwa mapokezi makubwa ikiwemomagari,pikipiki,katika uwanja wa ndege wa kia hadi viwanja vya tindigani kata ya kimandolu jijini Arusha siku ya jumamosi(kesho tarehe 15) ambapo atahutubia wananchi katika mkutano ulioandaliwa na chama
hicho.
Akizungumza mapema jana na waandishi wa habari katika ofisi za chama hicho juu ya maandalizi hayo Mwenyekiti wa chadema Mkoa wa Arusha Amani Golugwa alisema kuwa mapokezi hayo yamekamilika kwa asilimia miamoja na tukiohilo ni la kihistoria



Mwenyekiti wa chadema Mkoa wa Arusha Amani Golugwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya mapokezi ya mgombea Urais Edward Lowassa kupitia CHADEMA yamekamilika kwa asilimia miamoja na tukio hilo kuliita la kiistoria ambalo litafanyika katika viwanja vya tindigani kata ya kimandolu jijini Arusha siku ya jumamosi(kesho tarehe 15)(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)


Alisema kuwa lengo la ujio huo ni kumtambulisha mgombea urais ambaye ataambatana na mgombea mwenza Juma Duni Hajji ,kwa kuwatambulisha kwa wananchi wa Mkoa wa
Arusha sambamba na kupata udhamini wa wananchama waliojiandikisha kupiga
kura

Pia alisema kuwa zoezi la udhamini umeshaanza Arusha na uongozi wa Tume umaelekeza mgombea kupata wadhamini 300 na jimbo la Moshi mjini wataoa wadhamini 300

Aidha aliwataka ,wakazi wa jijili la Arusha na waliopo jirani kujitokeza kwa wingi katika tukiohilo
la kihistoria ambapo pia viongozi wakuu wa chama hicho watahudhuria akiwemo Mwenyekiti wa Taifa Freeman Mbowe,wenyeviti wenza wa ukawa
kutoka NLD,NCCR pamoja na chama cha CUF,John Mnyika ,Nibu katibu mkuuZanzibar Salum Mwalimu na viongozi wengine wengi.

“Kwakushirikiana na jeshi la polisi pamoja na vikosi vyetu suala la Amani,Utulivu,Ulinzi na Usalama
vitadumishwa katika msafara huo pamoja na mkutano huo”Alisema Golugwa
Hata hivyo baada ya mkutano huo kuisha msafara huo utaelekea katika jimbo la Monduli ambapo pia Mh.Lowassa atapata wasaa wa kuhutubia wananchi katika jimbo hilo
Kwa upande wake Naibu katibu mkuu waTimu Lowassa for president Ndama Jeuri alisema wamejiandaa vizuri kumpokea na wataendelea kuhamasisha watu kumuunga mkono Lowassa
katika harakati zake za Urais

Katika msafara huo zaidi ya magari 75 yataanzia katika ofisi za chadema hadi katika uwanja
wa ndege wa kia huku vikundi mbalimbali vya ngoma vikitumbuiza wakati wa
mapokezi ya Lowassa.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top