Mabalozi
wa mashina mia moja na kumi wa CCM,Mwenyekiti,Katibu kata, Wajumbe wa
kamati ya siasa ya kata pamoja na Wenyeviti wa mitaa minne katika kata
ya Monduli mjini mkoa Arusha wamehama CCM na kuhamia Chadema.
Tukio
ilo limetokea Monduli mjini jana majira ya saa sita mchana wakati
viongozi hao walipo kusanyika na kutoa kauli ya kuhama CCM na kuhamia
Chadema huku wakisema chama cha Mapinduzi kinaongozwa kibabe na
kimekosa mwelekeo.
Kwa
upande wao wenyeviti wa serikali za mitaa,wajumbe wa nyumba kumi na
katibu wa CCM kata ya Monduli Anna Erinest wameitaka jamii itambue kuwa
hayo ni maamuzi yao binafsi na hayahusiki na shinikizo la mtu yoyote
kama inavyo daiwa na baadhi ya watu kwamba kila wanaohama hudaiwa
wameshinikizwa.
Post a Comment