Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya
Takwimu Bw. Ephraimu Kwesigabo akitoa taarifa ya kuongezeka kidogo kwa
mfumuko wa bei nchini kwa mwezi Mei 2015 leo jijini Dar es
salaam.Mfumuko wa Bei wa bei kwa mwezi Julai ,2015 umefikia asilimia
6.4 kutoka asilimia 6.1 iliyokuwepo Juni 2015.
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
OFISI
ya Taifa ya Takwimu imetangaza Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Julai
2015 na kusema kuwa umeongezeka hadi kufikia asilimia 6.4 kutoka
asilimia 6.1 iliyokuwepo mwezi Juni 2015.
Hii
inamaanisha kuwa kasi ya upandaji wa bei ya bidhaa na huduma kwa
mwezi Julai 2015 imeongezeka ikilinganishwa na kasi ya upandaji bei ya
bidhaa na huduma iliyokuwepo mwezi Juni mwaka 2015.
Mkurugenzi
wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)
Bw. Ephraim Kwesigabo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es
salaam amesema kuongezeka huko kumesababishwa na kasi ya upandaji wa bei
ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula katika maeneo
mbalimbali nchini.
Amezitaja
bidhaa za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa mfumuko huo kutokana na
upandaji wa bei katika masoko kwa mwezi Julai 2015 kuwa ni mchele kwa
asilimia 27.9,mahindi asilimia 2.3, unga wa muhogo asilimia 9.2, nyama
asilimia 4.5, samaki 12.2, na maharage asilimia 5.9.
Kuhusu
Fahirisi za Bei ambacho ni kipimo kinachotumika kupima mabadiliko ya
bei ya bidhaa na huduma zinazotumiwa na kaya binafsi hapa Tanzania,
Kwesigabo amesema zimeongezeka hadi kufikia 158.78 kutoka 158:12 za
mwezi Juni.
Amesema
kuongezeka kwa fahirisi za bei kumechangiwa na ongezeko la bei ya
baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula zikiwemo gesi ya
kupikia kwa asilimia 3.7, mafuta ya dizeli 5.9, mafuta ya Petroli
ailimia 4.9, unga wa mahindi asilimia 2.5, ulezi asilimia 2.9, samaki
asilimia 4.8, viazi vitamu asilimia 2.6 na ndizi za kupika asilimia 3.4.
Kwesigabo
amesema uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na
huduma za mlaji kwa mwezi Julai , 2015 umefikia shilingi 62 na senti 98
ikilinganishwa na kiasi cha shilingi 63 na senti 24 za mwezi Juni
2015.
“Uwezo
wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma zilezile
kwa mlaji kwa mwezi Julai ,2015 na umepungua hii ina maana kuwa sasa
mtu anahitaji kuongeza ziada ya shilingi 38 ili aweze kununua bidhaa na
huduma sawa na zile alizokuwa na uwezo wa kuzinunua katika mwezi Juni"
Kwa
upande wa mfumuko wa Bei kwa nchi za Afrika Mashariki kwa mwezi Julai,
2015 Bw.Kwesigabo amesema kuwa una mwelekeo unaofanana , Kenya umepungua
kidogo hadi kufikia asilimia 6.62 na kutoka 7.03 mwezi Juni 2015 huku
Uganda ikiwa na mfumuko wa Bei wa asilimia 5.4 kutoka asilimia 4.9 za
mwezi Juni, 2015.
Post a Comment