MIKOA
10 ya Tanzania bara, Inatarajia kuombea amani na utulivu katika Uchaguzi Mkuu
unaotarajia kufanyika Oktoba 25 mwaka huu hapa nchini.
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya
Msama Promotions, Alex Msama mikoa hiyo itaiombea amani Tanzania kupitia muziki
wa Injili kupitia waimbaji mbalimbali wa
ndani na nje ya nchi.
Msama
alisema awali kabla ya mikoa hiyo kuombea amani uchaguzi Mkuu, Tamasha la
kwanza lenye dhamira hiyo litafanyika Oktoba 4 jijini Dar es Salaam.
“Tumeona
kuna umuhimu kuwashirikisha waimbaji wa nyimbo za Injili kumuomba Mungu
atuongoze katika uchaguzi Mkuu ambao unatakiwa kuwa huru na haki, ili
kufanikisha hayo kwa ufanisi nyimbo za kumuomba na kumtukuza Mungu zitumike ili
dua na sala zisikike mbinguni,” alisema Msama.
Msama
alisema Kamati yake bado inaendelea na mchakato wa kufanikisha maandalizi ya
tamasha hilo ambalo litaimarisha na kudumisha amani na utulivu ulioasisiwa na
baba wa Taifa Mwalim Julius Kambarage Nyerere.
Aidha
Msama alisema tamasha hilo litashirikisha waimbaji mbalimbali wakiwemo wa
Tanzania na nje ambao watasaidia
kufikisha ujumbe huo kwa Mungu.
Msama
alisema wananchi wajiandae kupata neno la Mungu kupitia waimbaji wa nyimbo za
Injili ambao watafanikisha mungu kusikia wanachohitaji wananchi.
Post a Comment