Mwenyekiti
Mpya wa Mashindano ya Miss Tanzania Juma Pinto akiongea na waandishi wa habari
leo jijini Dar es salaam.Kushoto ni msemaji wa kamati hiyo na Miss Tanzania
namba 2 mwaka 2006 Jokate Mwegelo.
Allen Mhina Na Ally Daud –
Maelezo
Kamati inayosimamia
mashindano ya Miss Tanzania Lino International Agency imepata Mwenyekiti na
wajumbe wapya watakaoandaa ,kuratibu na kusimamia mashindano ya urembo ya Miss
Tanzania.
Akiwatambulisha wajumbe hao
mbele ya waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam, aliyekuwa Mwenyekiti wa
kamati ya Miss Tanzania iliyomaliza muda wake Hashim Lundenga amesema
kuwa kamati mpya ndiyo itakayowajibika na shughuli zote zilizokuwa
zikifanywa na kamati ya awali.
Amesema kamati hiyo
itafanya kazi zake kwa kuzingatia sheria na vigezo vyote vya kimaadili ili
kuepuka ukiukwaji wa taratibu za mashindano hayo.
“Hatutamvumilia
mwanakamati yeyote atakayevunja miiko ya mashindano haya, sisi tutakuwa nyuma
tukiangalia kwa umakini”, amesema Bw. Lundenga.
Kwa upande wake Mwenyekiti
mpya wa kamati hiyo Juma Pinto ametoa pongezi za dhati kwa kamati
iliyomaliza muda wake na kuhaidi kukubaliana na mfumo unatumika kuratibu
mashindano hayo .
“Namshukuru Lundenga
kwa kunikabidhi nafasi hii ya mwenyekiti wa kamati ya miss Tanzania,
naahidi kuratibu mashindano haya kwa kuzingatia vigezo na masharti
yaliyowekwa ili kamati yangu iweze kukidhi haja ya mashindano haya”. Amesema.
Naye Msemaji Mkuu wa kamati
hiyo na aliyekuwa Miss Tanzania namba mbili mwaka 2006 Jokate Mwegelo,
ametoa rai kwa wasichana wa kitanzania wajitokeze kushiriki mashindano hayo kwa
kuonesha vipaji walivyonavyo na kupata ajira.
Mwishoni mwa mwaka
jana Mashindano ya Miss Tanzania yalikumbwa na mtafaruku wa ukiukwaji
wa maadili na vigezo vya mashindano na kulazimika kusimamishwa kwa muda na
Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA).
.
Post a Comment