Muuaji wa waandishi wawili wa kituo cha TV WDBJ, Vester Lee Flanagan, akitangaza katika kituo hicho kabla ya kufukuzwa kazi.
Mtangazaji wa kituo cha TV WDBJ, Alison Parker, enzi za uhai wake.
Mpiga picha, Adam Ward, enzi za uhai wake.
Watangazaji waliouawa (kushoto na kulia) wakiwa katika mahojiano ya moja kwa moja kabla ya kupigwa risasi na Vester Lee Flanagan.
...Vester Lee Flanagan akifyatua bastola yake.
Flanagan akiwa ameshika bastola wakati akifanya mauaji hayo.
...Gari la Flanagan limepaki katika jimbo la Virginia baada ya kujiua mwenyewe.
Polisi wakiwa eneo la tukio.
Eneo ambalo watangazaji walipokuwa wakiendesha kipindi hicho.
Wananchi wa jimbo la Virginia wakiwaombea marehemu hao.
Polisi nchini Marekani imesema muuaji wa waandishi wawili wa kituo cha TV WDBJ, Alison Parker na mpiga picha, Adam Ward nchini Marekani amefariki. Ujumbe unaoonekana kutumwa na mtu aliyekuwa na silaha nchini Marekani na kuwaua kwa risasi watangazaji hao wawili wa televisheni wakati wa matangazo ya moja kwa moja unaashiria kwamba alikuwa na uchungu kwa kinachoonekana kuwa ubaguzi wa rangi.
Vester Lee Flanagan, aliyefutwa kazi katika kituo hicho cha televisheni alifariki baada ya kujipiga risasi, saa chache baadaye.
Msimaizi wa kituo hicho cha televisheni alimtaja mshambuliaji huyo kuwa mtu asiyekuwa na furaha ambaye ilikuwa vigumu kufanya naye kazi.
(CREDIT: DAILY MAIL)
Post a Comment