Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja na aliyekuwa mwenyekiti mkoa wa Dar es Salaam John Guninita wametangaza leo kuachana na CCM na kujiunga Chadema.
Mgeja akionyesha ishara ya Chadema baada ya kutoa tamko la kujiuzulu.
Wanahabari wakichukua matukio katika hafla hiyo.
Baadhi ya makada wa CCM alioungana nao kujiunga na Chadema.…
Makada
hao wa CCM wametangaza kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Dar es
Salaam leo.
Wakizungumza
katika mkutano huo, makada hao wamesema wamechukua uamuzi huo baada ya
kubaini CCM imepoteza mwelekeo na kwamba kinaendeshwa kibabe tofauti na
misingi ya kuasisiwa kwake.
Wametolea
mfano wa kukiukwa kwa demokrasia kulikofanywa wakati wa mchakato wa
kutafuta mgombea urais wa chama hicho ambapo Dr John Magufuli aliteuliwa
kupeperusha bendera ya CCM.
Hatua
ya makada hao imekuja ikiwa ni siku moja tu tangu aliyekuwa mbunge wa
chama hicho jimbo la Sikonge, Said Nkumba atangaze kuachana na chama
hicho na kujiunga na Chadema.
Huo
ni mwendelezo wa matukio ya makada na wabunge chama hicho kuhamia
upinzani hasa Chadema kwani awali aliyekuwa waziri mkuu wa zamani Edward
Lowassa aliachana na CCM baada ya jina lake kukatwa na kamati ya
maadili ya chama hicho.
Wengine
waliohama CCM ni aliyekuwa mbunge wa Arumeru Magharibi, Goodluck Ole
Medeye, aliyekuwa mbunge wa Segerea, Makongoro Mahanga ambaye pia ni
naibu waziri Kazi na Ajira, aliyekuwa mbunge wa Kahama, James Lembeli,
aliyekuwa mwenyekiti wa wenyeviti wa CCM, Mgana Msindai na mbunge wa
viti maalumu anayemaliza muda wake Esther Bulaya.
Credit: GPL
Credit: GPL
Post a Comment