Tume
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imesema itatangaza matokeo ya urais ndani
ya siku tatu kwa sababu watatumia Mfumo wa Kusimamia Matokeo (RMS) ambao
utawawezesha kupokea, kujumlisha na kutangaza matokeo.
Licha
ya kutakiwa kisheria kutangaza matokeo hayo ndani ya siku saba, NEC
imebainisha kuwa mfumo huo utasaidia kuongeza kasi ya ukusanyaji wa
matokeo kutoka sehemu mbalimbali nchini na kuyatoa ndani ya siku hizo.
Akizungumza
na viongozi wa dini jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa NEC, Jaji
Damian Lubuva alisema maandalizi ya uchaguzi yanaendelea vizuri na muda
wowote vifaa vya uchaguzi vitawasili nchini.
Jaji
Lubuva aliwataka viongozi wa dini kuwasukuma waumini wao kwenda kupiga
kura siku ya uchaguzi na siyo kuwaelekeza mtu wa kumpigia kura.
Alisema wao wana wajibu mkubwa katika kujenga umoja kwa sababu wanaaminiwa na wananchi.
Alisema
uandikishaji katika daftari la kudumu la wapigakura lilifanyika kwa
mafanikio na NEC imeandikisha karibu watu milioni 24. Alisema kazi
inayoendelea sasa ni uhakiki wa taarifa kwenye daftari hilo.
“Jana
(juzi) nilikuwa Angola kwenye mkutano, viongozi wenzangu walitupongeza
kwa kuandikisha watu wengi kwa BVR ndani ya miezi mitatu licha ya kuwa
na mashine chache,”alisema
“Kenya
waliandikisha watu milioni 14 kwa kutumia mashine 30,000 walizokuwa
nazo, kwa hiyo tumefanya jambo kubwa, tunawataka nanyi viongozi wa dini
muwahimize waumini kwenda kupiga kura siku ya uchaguzi,” alisema
mwenyekiti huyo.
Uhakiki wa Daftari la Wapigakura
Jaji
Lubuva alisema uhakiki wa daftari la wapigakura ulioanza Agosti 7,
unalenga kutoa nafasi kwa wapigakura kuhakiki taarifa zao ili kuondoa
kasoro mbalimbali zilizojitokeza wakati wa uandikishaji.
Alikanusha taarifa zinazoihusisha tume hiyo na njama za kuficha taarifa za baadhi ya wapigakura.
Alisema
baadhi ya taarifa bado hazijaingia kwenye mfumo, kwa hiyo zile ambazo
hazijaonekana sasa zitaingia kwenye mfumo huo baada ya siku chache.
“Wananchi wataweza kupata taarifa zilizoko kwenye database (rekodi) kwa
kutumia simu zao kupitia ujumbe mfupi. Namba hiyo ni *152*00#,”
Post a Comment