Jeshi
la Polisi nchini Tanzania limesema kuwa litatoa tamko la jeshi hilo juu
ya Chama cha Mapinduzi kuzidisha muda wakati wa Uzinduzi wa Kampeni za
chama hicho wiki iliyopita.
Akizungumza
na waandishi wa habari wakati wa mdahalo wa wadau wa uchaguzi jana
jijini Dar es salaam Kamishna wa Mafunzo na Operasheni wa Jeshi la
Polisi CP Paul Chagonja amesema kuwa wanashughulikia suala hilo na muda
ukifika watatoa tamko.
Ameongeza kuwa ili uchaguzi uwe wa Amani ni lazima watu wote watimize wajibu wao.
Kwa
upande wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliwakilishwa na Jaji Mstaafu John
Mkwawa alivitaka vyama vya siasa kuzingatia maadili ya uchaguzi
waliosaini ili kulinda amani na kuepusha migogoro na uvunjifu wa Amani.
Kwa
upande wa mwakilishi toka chama cha ADC Mwanaisha Yemba alivitaka vyama
vyenye vikundi vya ulinzi kuwapa sare na alama maalum walinzi wao ili
watambuliwe na kila mtu ili wakifanya vujo iwe rahisi kutambulika.
Post a Comment