Saa chache baada ya Profesa Ibrahim Lipumba kutangaza kujiuzulu wadhifa wa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), ametoweka nchini.
Profesa
Lipumba aliondoka nchini baada ya kumaliza mkutano wake na waandishi wa
habari katika Hoteli ya Peacok jijini Dar es Salaam, ambako alitangaza
kujiondoa katika chama chake na katika Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa).
Taarifa
zilizopatikana, baada ya kumaliza mkutano na waandishi, alielekea
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), na aliondoka
nchini kwa kutumia ndege ya Shirika la Ndege la Rwanda (Rwanda Air).
Awali
kiongozi huyo ambaye alivaa suti ya ‘dark blue’ na shati jeupe alikuwa
apande ndege ya Shirika la Ndege la Kenya (KQ) 485, lakini alibadili
mwelekeo baada ya kufika uwanjani na kuamua kupanda Rwanda Air kuelekea
Kigali saa 9 alasiri.
Chanzo
cha uhakika kutoka uwanjani hapo, kilieleza kuwa Profesa Lipumba,
alifika saa 7:00 mchana akiwa na vijana wawili wa kiume ambao
walionekana kama walinzi wake.
Katika muda huo ambao Profesa Lipumba alikuwa katika taratibu za kuondoka, palikuwapo na ndege nne tu za kwenda nje ya nchi.
Vijana
hao ambao hawakujulikana majina yao, walikuwa wakifuatilia kila hatua
ya kile alichokuwa akikifanya Profesa Lipumba, huku yeye akionekana
mwenye wasiwasi na msongo mkubwa wa mawazo.
“Profesa
Lipumba anaonekana hayuko katika hali ya kawaida, anaonekana ni mtu
mwenye msongo wa mawazo, na pia ana wasiwasi kama vile kuna jambo
linamsumbua.
“Macho yake yalionekana ni mekundu mithili ya mtu aliyekuwa akilia kwa muda mrefu, huku uso wake ukionekana hauna furaha,” kilisema chanzo chetu.
Wakati
hayo yakiendelea, Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad,
amelazimika kukatisha shughuli za kiserikali alizokuwa nazo Zanzibar na
kwenda jijini Dar es Salaam kunusuru hali ya sintofahamu ndani ya chama
hicho.
“Ndiyo hivyo imeshatokea, lakini tayari katibu mkuu amekuja bara kuhakikisha mambo yanakaa sawa na chama hakiyumbi,” alisema kiongozi wa CUF ambaye hakupenda kutajwa jina.
Post a Comment