Mkuu wa
Mkoa wa Dar es salaam, Said Meck Sadiki akizungumza katika uzinduzi wa
semina ya mafunzo ya madereva wa mabasi yaendayo haraka (BRT) leo jijini
Dar es salaam, juu ya kuanza kwa kipindi cha mpito cha mradi huo
Oktoba mwaka huu, Semina itakayofanyika Agosti 23 mwaka huu jijini Dar
es salaam.
Waziri
Mkuu, tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na mgeni rasmi Hawa Ghasia
akizungumza katika uzinduzi wa mafunzo ya madereva wa mradi wa mabasi
yaendayo haraka (BRT) waliokaa mbele, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es
salaam, Said Meck Sadiki na kulia ni Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk.
Didas Masaburi.
Waziri
Mkuu, tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na mgeni rasmi Hawa Ghasia
aliyeshika mkasi akikata utepe kuzindua mafunzo madereva wa mabasi
yaendayo haraka (BRT) jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa mafunzo
yayo ya madereva.
Baadhi ya viongozi wa jeshi la polisi hapa nchini wakiwa na abiria katika basi la mwendo wa haraka jijini Dar es Salaam leo.
Mgeni
rasmi na Waziri Mkuu, tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na mgeni
rasmi Hawa Ghasia akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi
katika mradi wa mafunzo ya madereva wa mabasi ya mwendo wa haraka (BRT)
jijini Dar es Salaam leo.
Moja ya mabasi yaendayo mwendo wa haraka yakiwa barabarani katikati ya jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
Na Mwandishi wetu.
SERIKALI
imewataka madereva walioanza kupata mafunzo ya kuendesha mabasi
yatakayotumika katika mradi wa mabasi yaendayo haraka (BRT) kuzingatia
mafunzo hayo ya kihistoria hapa nchini.
Mafunzo hayo yaliyoanza jana ni moja ya matayarisho ya kuanza kwa mradi huo katika kipindi cha mpito mwezi Oktoba mwaka huu.
Akifungua
rasmi mafunzo hayo jana jijini Dar es Salaam, Waziri Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bi. Hawa
Ghasia aliwataka madereva hao kuyapokea kwa bidii na umakini mkubwa.
“Mafunzo
haya yatawapa fursa ya kuweza kufanya kazi kwenye miradi mingine ya BRT
kwani vigezo na mtaala wake ni wa kimataifa,” alisema wakati wa
maadhimisho hayo katika eneo la Ubungo
Waziri
Ghasia aliieleza kwamba mafunzo hayo ni ya kihistoria hapa nchini kwani
kwa mara ya kwanza watapatikana madereva wenye leseni za kimataifa na
kuwa mafunzo hayo yatahusu pia namna ya kuhudumia wateja.
“Madereva
hawa watajengewa weledi na nidhamu katika kazi yao ambayo kwa sasa
inalalamikiwa sana na wananchi wakilalamikiwa kwa utovu wa nidhamu na
kutotii sheria za barabarani,” alisema.
Kwa
upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Said Meck Sadiki alisema
kuzinduliwa kwa mafunzo hayo ni ushahidi wa dhamira ya serikali kutatua
kero ya usafiri na msongamano wa magari jijini humo kupitia mradi wa
BRT.
“Mradi
huu wa aina yake nchini na barani Afrika utatoa fursa mbalimbali za
uwekezaji na biashara kwa sekta binafsi ambayo ndio msingi wa maendeleo
ya nchi,” alisema.
Mafunzo
hayo kwa madereva wazalendo yanafanyika baada ya kushinda usaili ulio
endeshwa na wataalamu kutoka chuo cha ufundi stadi na mafunzo (VETA).
Jumapili
iliyopita kampuni ya watoa huduma wa ndani wa mradi huo, UDA-RT
iliendesha semina ya mafunzo kwa wahariri wa vyombo vya habari kuhusiana
na huduma za kipindi cha mpito za mradi huo.
Mradi huo
wa awamu ya kwanza unahusisha ujenzi wa kilometa 20.9 za barabara
maalum kutoka Kimara hadi Kivukoni; barabara ya Msimbazi kutoka Faya
hadi Kariakoo-Gerezani na sehemu ya barabara ya Kawawa kuanzia Magomeni
hadi eneo la makutano ya Morocco.
Post a Comment