Afisa habari wa TFF,Baraka Kizuguto.
TIMU
ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inatarajiwa kuondoka nchini siku ya
jumamosi usiku kuelekea Muscat Oman, kucheza mchezo wa kirafiki kabla ya
kuunganisha kuelekea Istambul Uturuki kwa kambi ya wiki moja.
Taifa
Stars imepata mwaliko wa kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Taifa ya
Oman tarehe 24 Agosti, 2015 usiku, ambapo baada ya mchezo huo timu
itasafiri kuelekea nchini Uturuki katika jiji la Istambul.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu nchini Oman (OFA) liliomba kucheza mchezo wa kirafiki
na Taifa Star kabla ya kuwavaa Turkemebistan katika mchezo wa kuwania
kufuzu kwa Kombe la Dunia Septemba 03, 2015 kwa bara la Asia, ambapo
kocha wake mkuu Mfaransa Paul Leguen aliomba kucheza na vijana wa
Charles Mkwasa kujiandaa na mechi hiyo.
Mara
baada ya mchezo huo Taifa Stars itaelekea Istambul katika mji wa Kocael
hoteli ya Kartepe kwa kambi ya wiki moja, ikiwa nchini Uturuki Stars
inatarajiwa kucheza michezo miwili ya kirafiki kabla ya kurejea nchini
kucheza na Nigeria Septemba 05, 2015 mchezo wa kuwania kufuzu kwa
fainali za Mataifa ya Afrika.
Kocha
mkuu wa Taifa Stars, Charles Mkwasa anatarajiwa kutoa orodha ya kikosi
chake cha wachezaji 22 mwishono mwa wiki watakaosafiri kuelekea nchini
Uturuki kwa kambi ya hiyo ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Nigeria.
Mshambuliaji
Adi Yussuf anayechezea klabu ya Mansfield Towny ya Uingereza
alitarajiwa kujiunga na timu nchini Uturuki, lakini kutokana na majeruhi
aliyoyapata hivi karibuni katika michezo ya ligi, uongozi wa Mansfield
umeomba mchezaji huyo kutojiunga na timu ya Taifa kwa ajili ya kupata
mataibabu zaidi.
Adi
aliumia wiki iliyopita katika mchezo dhidi ya Nottingham Forest ambapo
kwa sasa anaendelea na matibabu chini ya uangalizi wa klabu hiyo, na
pindi atapokuwa fit atapata nafasi ya kujumuika na kuitumika timu ya
Taifa ya Tanzania.
Post a Comment