VYAMA vya siasa vinavyotakiwa kushiriki kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka huu baadaye Oktoba 25 mwaka huu ni 22.
Taarifa
iliyotolewa na Msajili wa Vyama vya Siasa jana Dar es Salaam na
kusainiwa na Msajili Msaidizi, Sisty Nyahoza, imetaja idadi hiyo ya
vyama vyama hivyo, ambavyo ni vyenye usajili wa kudumu kuwa ni ni Chama
Cha Mapinduzi (CCM), Chama cha Wananchi (CUF), Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), Union for Multiparty Democracy (UMD) na Chama cha
NCCR-Mageuzi.
Vingine
ni National League for Democracy (NLD), UnitedPeoples’ Democratic Party
(UPDP), National Reconstruction Alliance (NRA), African Democratic
Alliance Party (TADEA), Tanzania Labour Party (TLP) na United Democratic
Party (UDP).
Vyama
vingine ni Demokrasia Makini (Makini), Chama cha Haki na Ustawi
(Chausta), Democratic Party (DP), African Progressive Party of Tanzania
(APPT-Maendeleo) na Jahazi Asilia.
Vile
vile kuna chama cha Sauti ya Umma (SAU), Tanzania Farmers Party (AFP),
Chama cha Kijamii (CCK), Alliance for Democratic Change (ADC), Chama cha
Ukombozi wa Umma (Chaumma) na Alliance for Change and Transparency
(ACT-Wazalendo).
Post a Comment