Na Mwandishi Wetu
WAKATI
vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kesho vitazindua
kampeni zake za urais kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu
kwenye Viwanja vya Jangwani, Dar, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa ameitwa na wazee wa nyumbani
kwao, Karatu mkoani Arusha, Uwazi Mizengwe limedokezwa.
Chanzo
kilicho karibu na kiongozi huyo mwenye mvuto na ushawishi kisiasa
ambaye kwa sasa yupo katika ‘mgogoro’ na chama chake, kimesema Dk. Slaa
aliitwa ili kuweka mambo sawa kufuatia sintofahamu inayoendelea kati
yake na viongozi wenzake wa Ukawa tangu ujio wa kada wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Edward Ngoyai Lowassa ambaye ni mgombea wa urais
kupitia Ukawa.
Inadaiwa
kuwa baada ya kuwa kimya kwa wiki kadhaa akiwa nyumbani kwake Mbweni,
nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, kiongozi huyo alikerwa na wageni wa
aina mbalimbali waliokuwa wakifika nyumbani kwake kwa kupishana, wengi
wao wakienda kwa lengo la kumshawishi ili atangaze uamuzi wake kuhusu
siasa kitu ambacho hakuwa tayari kukifanya kwa wakati huo.
MANENO YA CHANZO
“Kama
wiki mbili mbili zilizopita, Dk. Slaa aliondoka Dar es Salaam kwenda
mapumzikoni katika Mbuga ya Wanyama ya Serengeti iliyopo mkoani Mara
ambako aliandamana na familia yake.”
Mizengwe: Samahani. Unaposema aliongozana na familia yake, una maana na mkewe, Josephine?”
Chanzo:
“Mimi sijui hilo. Elewa alikwenda na family yake. Lengo la safari yake
ni kupata nafasi nzuri ya kutafakari mustakabali wa maisha yake kisiasa.
Hapa Dar aliona anakosa utulivu kutokana na kupata wageni mara kwa
mara. Wanaingia na kutoka.”
Mizengwe: “Ni akina nani? CCM, Chadema, Ukawa au ndugu, jamaa na marafiki?”
Chanzo:
“Sijui…sijui! Sasa akiwa kule, wazee wa nyumbani kwao (Karatu)
wakasikia, wakaona ni wakati muafaka kwao kumuita na kuweza kuzungumza
naye ili kwanza wajue msimamo wake, lakini pia waone kama wanaweza
kumshauri lolote la kufanya katika kipindi hiki ambacho nchi inaingia
katika uchaguzi mkuu na kampeni zimeshaanza.”
BADO YUPO KARATU
Inadaiwa
kuwa kwa zaidi ya wiki moja sasa, Dk. Slaa yupo Karatu ambako
mazungumzo kati yake na wazee wa huko yanaendelea. Upo uwezekano mkubwa
wa kutokuwepo jijini Dar (kesho) wakati Ukawa watakapoanza kampeni zao
kumnadi mgombea wa urais ambaye ni Lowassa.
WAZEE WAGAWANYIKA
“Lakini
kinachoonekana ni kwamba, hata kule nyumbani kwao nao wazee
wamegawanyika. Wapo wanaomtaka dokta ahamie CCM na wengine wanamtaka
kurejea kuendelea na harakati za kuijenga Chadema. Lakini hadi hapa
ninapozungumza na wewe, bado hakuna uhakika juu ya uamuzi wa Dk. Slaa.”
Chanzo.
Chanzo
kikaendelea kudai kuwa, wazee hao walimwambia maisha yake ni ya siasa
hivyo kujitenga kwake kunaweza kuirudisha nchi katika enzi zisizokuwa na
ushindani wa vyama vingi. Walimwambia atafakari upya kwa sababu kuwa
kwake nje ya Chadema kuna msururu wa watu wengine nyuma yake.
DOKTA KIMYA
Kikaendelea: “Lakini dokta kama kawaida yake. Bado hasemi chochote, yeye si mtu wa kukurupuka. Si unamjua! Hajatoa jibu.”
UKAWA JANGWANI
Wakati
huohuo, kesho Ukawa watazindua kampeni zao kwenye Viwanja vya Jangwani
huku viongozi wawili waandamizi na waanzilishi wakiwa wamejiweka kando.
Viongozi
hao ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (Cuf), Profesa
Ibrahim Lipumba aliyejiuzulu nafasi hiyo wiki chache zilizopita na Dk.
Slaa. Wote wakidaiwa kutoridhishwa na mchakato wa kumkaribisha waziri
mkuu wa zamani, Edward Lowassa na kisha kupewa nafasi ya kugombea urais.
WITO WA DK. SLAA
Tangu
Dk. Slaa ajiweke kando, maneno mengi yamekuwa yakisemwa kuhusu padri
huyo wa zamani, lakini mara zote amewataka Watanzania kuwa wavumilivu
kwani wakati muafaka ukifika, ataeleza kilichomo moyoni mwake.
Uwazi
Mizengwe juzi lilimtafuta Dk. Slaa kwa njia ya simu bila mafanikio.
Hata lilipofika nyumbani kwake, mwenyeji mmoja aliyegoma kujitambulisha,
alisema kiongozi huyo yupo nje ya jiji kwa shughuli zake binafsi.
chanzo:uwazimizengwe
Post a Comment