CHAMA
Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam jana kimetangaza majina ya
wagombea udiwani katika majimbo 10 ya uchaguzi huku ikiwaengua, Yussuf
Manji na Diwani wa Kata ya Jangwani Abuu Jumaa.
Katibu
wa Siasa na Uenezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba alitangaza
wagombea wa udiwani kwa tiketi ya CCM wa kata 91 huku kata moja ya
Mianzini katika Jimbo la Mbagala uchaguzi wake utafanyika baadaye baada
ya ule wa wali kuvurugika.
“
Kwa mujibu wa Katiba ya CCM, Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa ndiyo yenye
dhamana ya kupitisha majina ya wagombea wa nafasi ya udiwani, baada ya
kupokea majina na baadaye kupitia na kuhakiki malalamiko yote,” alisema Simba.
Katika
kata ya Mbagala Kuu ambayo Mwenyekiti wa Yanga, Manji aliongoza katika
kura hizo alikatwa na Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam
kutokana na kukosa sifa na nafasi kuchukuliwa na mgombea aliyeshika
nafasi ya pili Abubakari Othuman.
Kwa
upande wa kata ya Jangwani ambayo wananchi walilalamika Diwani wa kata
hiyo, Jumaa kwa kuongoza tangu enzi za utawala wa awamu ya kwanza, jina
lake limekatwa na kupitishwa la mgombea aliyeshika nafasi ya pili Abdul
Faraji.
Aidha,
akizungumza malalamiko ya wanachama wa CCM kata ya Mbagala Kuu ambao
walifika ofisini hapo kwa basi maalumu kupinga kuenguliwa, Mwenyekiti wa
CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida alisema Manji amendolewa
kutokana na kukosa sifa.
“
Manji hakutokea kuchukua fomu wala kurudisha fomu, lakini hilo sio
tatizo, wakati wa kampeni tuliweka utaratibu wa wagombea kutumia usafiri
mmoja kwenye kuomba kura kwenye matawi, Manji hakushiriki. “
Hata
wakati wa vikao vya mchujo vya Sekretarieti na kamati ya usalama na
maadili ngazi ya kata na wilaya, Manji hakutokea na alipopigiwa simu
alijibu amelala.
Alisema
kutokana na kutofuata taratibu hizo Manji anakosa sifa za kuwania
nafasi ya udiwani, kuwa kura alizopata amezipata kwa hila hivyo sio
halali.
“Tulipokaa
kwenye mchujo katika sekretarieti na kamati ya usalama na maadili ngazi
ya mkoa, Manji pia hakutokea na hapo ndipo yalipokuja malalamiko ya
wagombea wenzake kuwa mtu akiwa na fedha anaweza kulala nyumbani kwake,
asipige kampeni na akapewa nafasi ya kugombea,” alisema.
Post a Comment