Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
WADHAMINI
wakuu wa klabu kongwe nchini, Bia ya Kilimanjaro, leo 'wamezipamba
maua' baada ya kuzikabidhi jezi na vifaa vingine vipya vyenye thamani ya
Sh. milioni 70 kwa ajili ya msimu huu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara (VPL) utakaoanza Septemba 12.
Akizungumza
wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa hivyo jijini Dar es Salaam leo
asubuhi, Meneja wa Kilimanjaro Premium Lager, Pamela Kikuli, amesema
wataendelea kuhakikisha mishahara ya wachezaji wa klabu hizo mbili
inalipwa huku wakijivunia kuzinunulia klabu hizo mabasi mawili makubwa
kwa ajili ya usafiri wa wachezaji.
"Tunaamini
timu zote mbili zimesajili vizuri na zitafanya vyema kwenye ligi msimu
huu. Yanga imetwaa Ngao ya Jamii na Simba imekuwa ikifanya vizuri katika
mechi za kirafiki tangu kuajiriwa kwa kocha mpya," amesema Pamela.
Vifaa
vilivyokabidhiwa leo kwa wawakilishi wa klabu hizo; Kaimu Katibu Mkuu
wa Simba, Collins Frisch na Meneja Masoko wa Yanga, Omary Kaya ni jezi
seti mbili kwa kila klabu, jezi za mazoezi, 'casual wear', mipira,
vizuia ugoko (sheen guard), viatu vya kuchezea, viatu vya mazoezi,
soksi, glavu za makipa na mavazi ya maofisa wa mabenchi ya ufundi.
Wawakilishi
wa klabu hizo mbili wameupongeza uongozi wa Kilimanjaro Premium Lager
kwa kuwapatia vifaa hivyo huku wakiomba ufadhili zaidi kutoka kwa wadau
wengine wa michezo nchini.
Post a Comment