Chama cha Mapinduzi kinapenda kutoa taarifa kuhusu masuala kadhaa.
Mwenendo wa Kampeni
Kwa kifupi, Mgombea Urais, Ndugu John Pombe Magufuli na Mgombea-Mwenza Ndugu Samia Suluhu Hassan, wanaendelea vizuri na kampeni.
Kila mmoja anafanya mikutano na wananchi kati ya 8 hadi 11 kwa siku na kukutana na maelfu kwa maelfu ya wananchi.
Tunawashukuru wananchi wanaokuja kwenye mikutano yetu. Tunawashukuru pia makada wa CCM wanaojitolea kwa hali na mali kukipigania Chama cha Mapinduzi na kumtafutia kura Ndugu Magufuli.
Tunawashukuru wananchi wanaokuja kwenye mikutano yetu. Tunawashukuru pia makada wa CCM wanaojitolea kwa hali na mali kukipigania Chama cha Mapinduzi na kumtafutia kura Ndugu Magufuli.
Tunaridhika
sana na mwenendo wa kampeni yetu. Katika nusu hii ya pili ya kampeni
tutaongeza kasi na msukumo wa kuwafikia wananchi wengi zaidi kwa mbinu
na mikakati mipya.
Midahalo ya Wagombea
CCM inapenda kusisitiza yafuatayo:
Midahalo ya Wagombea
CCM inapenda kusisitiza yafuatayo:
1. Ndugu Magufuli amekubali kushiriki mdahalo wa wagombea Urais
2. Mdahalo uwashirikishe wagombea wenyewe na sio wawakilishi wao.
3.
Wagombea wote, hasa wa vyama vikuu, wawepo na washiriki.
Tunapozungumzia mabadiliko katika nchi maana yake ni utayari wa kufanya
mambo mapya yenye tija ambayo hayajawahi kufanyika, ikiwemo mdahalo wa
wagombea Urais. Wanaohubiri mabadiliko huku wakiogopa kushiriki mdahalo
wanahubiri mabadiliko hewa.
UTAFITI WA TWAWEZA
CCM haikushangazwa na matokeo ya utafiti wa taasisi huru ya Twaweza yaliyotangazwa jana ambayo yanatoa ushindi wa asilimia 65 kwa Ndugu John Pombe Magufuli dhidi ya asilimia 25 za Mgombea wa UKAWA. Hatukushangazwa na matokeo ya utafiti huu kwasababu tano:
CCM haikushangazwa na matokeo ya utafiti wa taasisi huru ya Twaweza yaliyotangazwa jana ambayo yanatoa ushindi wa asilimia 65 kwa Ndugu John Pombe Magufuli dhidi ya asilimia 25 za Mgombea wa UKAWA. Hatukushangazwa na matokeo ya utafiti huu kwasababu tano:
1.
Siku UKAWA walipomteua Ndugu Edward Lowassa kuwa mgombea wao ndio siku
CCM ilipohakikishiwa ushindi katika uchaguzi wa mwaka huu. CCM
hatukumteua kwasababu tuliamini hakuna namna ambapo Watanzania wengi
watamchagua.
2.
Katika uchaguzi wa mwaka huu CCM tunafanya utafiti wetu wa ndani wa
kisanyansi kila wiki kujua mwenendo na mwelekeo wa kampeni na maeneo
yanayohitaji nguvu mahsusi. Tangu tuanze utafiti wetu mwishoni mwa mwezi
Agosti, karibu kila wiki asilimia za ushindi wa CCM hazijawahi kushuka
chini ya asilimia 60 na zimekuwa zinapanda.
3.
Kazi kubwa anayofanya mgombea wetu, Ndugu John Pombe Magufuli, na
mgombea-mwenza, Ndugu Samia Suluhu Hassan, kuzunguka nchi nzima kwa
barabara na kuongea moja kwa moja na wapiga kura inazaa matunda.
Wanawafikia wapiga kura wengi, hasa wa vijijini, na wapiga kura hao
wanawaelewa.
4.
Kampeni kubwa zinazofanywa na wagombea Ubunge na Udiwani wa CCM na
makada na viongozi wa Chama katika ngazi zote nchi nzima kila siku
kumuombea kura Magufuli nazo zinazaa matunda.
5.
Tunaamini pia migogoro ndani ya UKAWA katika kipindi hiki cha uchaguzi
iliyopelekea mitafaruku katika kuachiana majimbo na, baadaye, kutokana
na uteuzi wa Mgombea Urais wa UKAWA, kupelekea kujiuzulu kwa viongozi wa
muda mrefu na maarufu wa UKAWA, Profesa Ibrahim Lipumba na Dr. Wilbrod
Slaa, na migongano ndani ya NCCR-Mageuzi, yote haya yamepunguza imani ya
wananchi kuhusu uwezo wa vyama hivi kushika dola.
Lakini
vilevile matokeo ya utafiti huu ni ishara kwamba Watanzania wamempokea
na kumuelewa Ndugu Magufuli na wako tayari kumkabidhi nchi.
Sisi kama CCM kuna baadhi ya mambo tumeyachukua katika utafiti huu na tutayafanyia kazi ili kujihakikishia ushindi. Tumeshangazwa na taharuki, hasa kutoka miongoni mwa wasomi na wanaharakati, kuhusu matokeo ya utafiti huu.
Sisi kama CCM kuna baadhi ya mambo tumeyachukua katika utafiti huu na tutayafanyia kazi ili kujihakikishia ushindi. Tumeshangazwa na taharuki, hasa kutoka miongoni mwa wasomi na wanaharakati, kuhusu matokeo ya utafiti huu.
CCM
ilitegemea kwamba jamii ya wasomi na wanaharakati ingefurahia utamaduni
wa tafiti za kisiasa unaoanza kujitokeza hapa nchini ili siku zijazo
tujikite katika kurekebishana kwenye kanuni za utafiti na ithibati na
uhakiki wa ubora. Tunasikitika kwamba yanawekwa mazingira ya kutisha na
kukatisha tamaa (atmosphere of intimidation) kwa watu wanaotaka kufanya
tafiti za kisiasa nchini.
Utafiti
ni sayansi. Matokeo ya utafiti hupingwa kwa matokeo ya utafiti
mwingine, sio kwa kuponda tu au kwa matusi na vitisho. Ni vyema
tukajifunza kupokea habari mbaya bila taharuki. Itakumbukwa kwamba,
mwezi Agosti 2010, taasisi ya utafiti ya kimataifa ya Synovate ilitoa
utafiti ikionyesha kwamba CCM itashinda Uchaguzi Mkuu wa 2010 kwa
asilimia 61.
Baadhi
ya wana-CCM hawakufurahishwa na matokeo ya utafiiti huo kwasababu
waliamini kwamba ushindi wetu ulikuwa ni mkubwa zaidi. Wapinzani
waliwalaani, kuwatukana na hata kutaka kuwashtaki Synovate. Kwenye
matokeo halisi ya kura, CCM ilipata asilimia zilezile 61 zilizotabiriwa
na Synovate.
Ni vyema kuweka akiba ya maneno kwenye masuala haya.
Imetolewa na:
January Makamba
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya CCM
23.09.2015
Post a Comment