Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Godbless Lema Aachiwa Kwa Dhamana.

\

Mgombea ubunge jimbo la Arusha Mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Godbless Lema na wenzake wanne wameachiliwa kwa dhamana jana baada ya kushikiliwa na polisi  juzi.

Polisi mkoani Arusha walimkamata mwanasiasa huyo pamoja na watu wengine wanne juzi jioni mara baada ya kuzindua kampeni yake ya kuwania ubunge katika jimbo hilo kwa awamu ya pili katika Shule ya Msingi Ngarenaro.

Wakisomewa mashtaka katika mahakama ya Arusha, Lema amedaiwa kulizima gari lake wakati wakitokea kwenye mkutano wa kampeni, hali iliyowafanya wafuasi wake kuanza kulisukuma hivyo kusababisha maandamano pasipo kuwa na kibali cha polisi. Lema na wenzake wameyakana mashtaka dhidi yao.

Mwanasiasa huyo na wenzake wameachiwa huru baada ya kutimiza masharti ya dhamana waliyowekewa.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top