Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

HAKUNA CHAMA CHA TANZANIA PEOPLE’S PARTY (TPP)-NYAHOZA


 Msajili  Msaidizi wa ofisi ya msajili  wa Vyama  vya Siasa, Sisty Nyahoza akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya kuufahamisha umma kuwa chama cha siasa Tanzania Peoples Party (TPP) kilifutwa kwenye orodha ya vyama vya siasa hapa nchini na chama hicho hakipo kwenye orodha ya vyama vya siasa vilivyopo hapa nchini amesema hayo  wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, kushoto ni Mkurugenzi Utawala na Rasilimali watu Emmanule Kayuni,.
Wanahabari wakimsikilza kwa makini Msajili  Msaidizi wa ofisi ya msajili  wa Vyama  vya Siasa, Sisty Nyahoza leo Jiji Dar es Salaam.
 (Picha na Emmanue Massaka).
 
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
OFISI ya Msajili wa Vyama vya Siasa imesema kuwa Chama cha Tanzania People’s Party (TPP) kilifutwa, hivyo hakuna mtu mwenye mamlaka ya kutumia chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
 
Akizungumza na waandishi habari leo jijini Dar es Salaam, Msajili Msaidizi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza amesema kuwa hivi karibuni kuna watu wameonekana katika chombo cha habari kimoja  sio Michuzi, wakiwajinasibu katika chama cha TPP wakati chama hicho kilishafutwa  toka 2001.
 
Nyahoza amesema kuwa watu wanaotumia chama hicho sheria itashika mkondo wake kwa kuwachukulia hatua watu kutumia chama ambacho kilishafutiwa usajili wa kudumu kwa msajili wa vyama vya siasa.
 
Aidha amesema kuwa vyama vilivyo katika usajili wa kudumu na vimeshiriki uchaguzi mkuu ni vyama 22 hivyo watu watambue chama cha TPP kilishafutwa kutokana na kukiuka kwa taratibu za ofisi ya msajili wa vyama vya siasa.
 
Nyahoza amesema kuwa watu wote wanaotumia vyama ambavyo usajili wake ulishafutwa  kwa mamlaka ya ofisi ya msajili wa vyama vya siasa watatachukuliwa hatua.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top