Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM,Ndugu
Abdallah Bulembo ambaye pia ni Kiongozi wa msafara wa kampeni za Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi
CCM,akiwaongoza baadhi ya viongozi mbalimbali wa chama hicho na wageni
waalikwa kutoka Serikali ya Mkoa wa Geita kukata Ndafu ikiwa ni sehemu
ya kusherehekea sikukuu ya Eid El Hajj kwa pamoja,wakati wa mapumziko
ya shughuli za kampeni za Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe
Magufuli,ambapo leo alitarajia kuendelea na kampeni zake mkoani
Shinyanga.
Wakati
huo huo Mgombea urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia tiketi
ya Chama Cha Mapinduzi CCM Dr.John Magufuli ameahirisha mikutano yake
ya kampeni aliyokuwa aifanye leo Mkoani Shinyanga ili kupisha sikukuu ya
Eid El Hajj,pia amewatakiwa Watanzania wote popote pale walipo sikukuu
njema na yenye Baraka mbele za Mwenyezi Mungu na na kuwa tuendelee
kuidumisha Amani ya Nchi yetu.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya
CCM,Ndugu Abdallah Bulembo ambaye pia ni Kiongozi wa msafara wa kampeni
za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania kupitia chama cha
Mapinduzi CCM,akizungumza jambo mbele ya baadhi ya viongozi mbalimbali
wa chama hicho na Serikali ya Mkoa wa Geita wakati wa mapumziko ya
kusherehekea sikukuu ya Eid El Hajj kwa pamoja,mapema le mchana mkoani
Geita
Ndafu akiwa ameandaliwa tayari kwa kuliwa.
Ndafu ikikatwa kwa pamoja.PICHA NA MICHUZI JR-GEITA.
Post a Comment