Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

KIKWETE AIPONGEZA BRELA KWA USAJILI WA KISASA


 Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Rais Jakaya Kikwete (Pichani)ameridhishwa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) kwa hatua iliyofikiwa ya kuweza kusajili jina la biashara kwa njia ya mtandao na kupata cheti ndani ya saa moja.

“Hatua hii ya BRELA ni nzuri, wanastahili pongezi na wengine waige,” alisema Dkt. Kikwete kwenye mkutano wa Nane wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

Pongezi za Dkt. Kikwete zilikuja wakati wa kipindi cha majadiliano juu ya kuboresha mazingira ya kufanya biashara nchini ambapo alijulishwa maendeleo hayo na Ofisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Bw. Frank Kanyusi.
 
Akithibitisha maendeleo hayo mmoja wa washiriki wa mkutano huo kutoka VIBINDO alisema hivi karibuni aliweza kufanikiwa kusajili jina la biashara kwa kipindi cha saa moja tu.
 
BRELA imeanza mfumo huo wa kusajili jina la biashara kupitia mtandao mwezi Juni mwaka huu.
 
Mteja wa BRELA anayetaka kusajili jina la biashara anatakiwa kuwa na jina analopendekeza, anuani ya barua pepe, kitambulisho cha taifa, pasi ya kusafiria, kitambulisho cha kupigia kura au leseni ya gari, namba ya simu na kufahamu tarehe yake ya kuzaliwa.
 
Mteja anatakiwa kuingia katika mtandao wa BRELA ambao ni www.brela.go.tz kisha ataingiza jina na baada ya jina kukubalika, atapata nyaraka ya malipo yenye namba ya kulipia.
 
Baada ya hapo, mteja atachukua namba ya malipo kwenye nyaraka hiyo na kwenda kulipia benki za NMB au CRDB na baadaye kuingiza namba ya malipo yake katika kumalizia mchakato huo wa kimtandao.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top