Mgombea kiti cha Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kupitia vyama vinavyounda UKAWA, Mh. Edward
Lowassa, leo tena amelitikisa jiji la Dar es Salaam, hususan maeneo ya
Kibamba kulikofanyika mkutano wa kihistoria wa kampeni ambapo maefu ya
wananchi walifurika wengine wakikaa juu ya mapaa ya nyumba za madarasa,
wengine kwenye miti, kutokana na kukosa eneo zuri la kuweza kushuhudia
"live" mkutanonukiendelea. Changamoto ya maeneo ya kufanyia mikutano ya
kampeni ndiyo inayoonekana kuikumba UKAWA, kutokana na kuongezeka kwa
idadi ya watu wanaohudhuria mikutano hiyo. Pichani mfuasi wa UKAWA,
akiwa amejichora rangi za bendera ya CHADEMA akiambatanisha maneno
maarufu yanayotumiwa na wafuasi wa Mh. Lowassa kwa sasa, yaani "Ulipo
tupo".
Mh. Lowassa na viongozi wengine wa UKAWA, wakiwa jukwaani mbele ya umati wa watu
Wananchi wakionyesha alama ya mabadiliko inayotumiwa hivi sasa na UKAWA
Mh. Lowassa, na Mwenyekitin wa CHADEMA, Mh. Mbowe, wakiwasili kwenye eneo la mkutano huko Kibamba










Post a Comment