Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Mgeja Ashangaa Push-Up Za Magufuli....Asema Anafaa Kushiriki Michezo Ya Olympic Na Sio Urais



Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja  ambaye  alijiondoa  na  kuhamia  Vyama pinzani, amesema anashangaa kuona mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli, akipiga push up, hivyo akasema anafaa kushiriki michezo ya Olympic na siyo kuwa rais.

Mgeja aliitoa  kauli  hiyo jana  wakati wa mkutano wa kampeni za Lowassa uliofanyika katika ngome ya Katibu wa Itikadi na Uenezi ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, Jimbo la Mtama  
 
Alisema mgombea ubunge wa CCM katika jimbo hilo, Nape anamfahamu na hajawahi kushinda uchaguzi wowote.

"Mna bahati mbaya sana hapa Mtama, sisi tunamwita .... amekumbuka shuka (kwao) wakati kumekucha," alisema na kuongeza Nape siyo mkazi wa Mtama na anakuja jimboni humo akiwa na brief case na kulala nyumba ya wageni kuomba kura.

Akimjibu Mzee John Malecela, aliyesema waliotoka CCM wana matatizo, Mgeja alisema waliotoka CCM ni watu safi.

"Sisi tuliotoka CCM ni watu safi kabisa, ukiwa mchafu CCM huwezi kutoka," alisema.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top