Shani Ramadhani
Mtoto Violeth akiwa na mama
yake.Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, Rose alisema, baba
yake mzazi alimlazimisha kuolewa akiwa na umri wa miaka 14 baada ya
kuhitimu elimu ya darasa la saba, mwaka 2010.“Baada ya kuolewa nikaanza kunyanyaswa
kwa kufanyishwa kazi ngumu kama kulima, kuchunga mifugo na nyingine
nyingi. Baadaye nikapata ujauzito wa kwanza, nikalea ile mimba kwa
tabu.
“Siku ya kujifungua
nikapelekwa hospitali lakini sikujifungua, mume wangu akaamuru
nirudishwe nyumbani ambapo nikawa napewa dawa za kienyeji kwa kuwekewa
puani, mdomoni na sehemu za siri,” alisema Rose.Rose aliendelea
kusimulia kuwa, baada ya kutumia dawa hizo hali yake ikawa mbaya,
akarudishwa tena hospitali na kufanyiwa vipimo ambapo iligundulika mtoto
alifia tumboni. Kwa kutumia mikasi, madaktari wakamtoa mtoto.
Rose hakuishia hapo,
aliendelea kuliambia Uwazi kuwa, alipata ujauzito wa pili ambao
aliteseka nao sana kwa kufanya kazi ngumu kiasi kwamba ilibidi arudi kwa
baba yake ambaye naye alimfukuza.
“Nilirudi kwa mume wangu
mpaka nilipojifungua. Nilishtuka sana kujifungua mtoto mwenye magamba
mwilini. Niliporudi nyumbani nikakuta mume wangu ana mwanamke mwingine.
Alivyoniona na huyu mtoto akaniambia nichague mawili. Niondoke kwake au
mimi na mwanangu tuuawe.
“Ilibidi niondoke. Nikaanza
kuombaomba pesa kwa wasamaria wema kwa ajili ya kumpeleka mtoto
Hospitali ya Bugando kwa matibabu. Nilipofika, nilipata wakati mgumu kwa
sababu sikuwa na mahali kwa kufikia.
“Ilikuwa nikipata mtu wa
kunisaidia pa kulala, nakwenda naye lakini ikifika asubuhi huyo mtu
akimwona mwanangu vizuri ananifukuza. Nikawa nahangaika mpaka nikaja
kukutana na msamaria mwema mwingine ambaye hadi sasa naishi kwake na
mwanangu.
“Hospitali wamenipa
masharti ya namna ya kumtunza mwanangu kwamba nimpe chakula bora, mafuta
yasiyo na harufu na kumbadilisha nguo mara kwa mara kwa siku.“Naomba
Watanzania wanisaidie pesa nipange chumba na kupata mtaji wa biashara
ndogondogo kwa ajili ya kuniwezesha kumtunza huyu mtoto,” alisema Rose
kwa huzuni.
Naye Ibanda Manyonyi
aliyejitolea kumhifadhi mama Violeth alisema yeye aliamua kuchukua
uamuzi huo kwa sababu Mungu amembariki kuwa na uzima japo hana uwezo wa
kipesa.
“Kutokana na hali ya
mwanaye ilivyo na alivyokuwa ananyanyasika na watu hapa mjini, mimi
sikuona sababu ya kumuacha aendelee kuteseka na mtoto mdogo hivi ndiyo
maana nikaamua niishi nao kama binadamu wenzangu,” alisema Manyonyi.
Kwa yeyote atakayeguswa na habari ya mama huyu awasiliane naye kwa namba 0757-665556.
Picha kwa hisani ya Nitetee Foundation kupitia kipindi cha Nitetee Sauti ya Mnyonge kinachorushwa Star TV.
Post a Comment