Msanii
wa Reggae Princes Delyla akiongea na wadau wa Sanaa kwenye Jukwaa la
Sanaa la Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) mapema wiki hii kwenye makao
makuu ya Baraza hilo Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam. Kulia
kwake ni Msanii Mwasiti Almas na Afisa Sanaa kutoka BASATA Augustino
Makame.
Msanii
wa kizazi kipya Mwasiti Almas(katikati) akisisitiza jambo wakati
akiongea na wadau wa Sanaa kwenye programu ya Jukwaa la Sanaa la Baraza
la Sanaa la Taifa (BASATA) linalofanyika makao makuu ya Baraza hilo
Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Msanii wa
reggare Princes Dalyla na Afisa Sanaa kutoka BASATA Augustino Makame.
Mtafiti
na Msanii wa Reggae Innoncent Nganyagwa akifafanua jambo kwenye Jukwaa
la Sanaa la Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) mapema wiki hii. Kulia
kwake ni Msanii mwenzake wa Reggae Princes Delyla.
Msanii Mwasiti akisakata muziki sambamba na mashabiki wake kwenye Jukwaa la Sanaa la BASATA.
Msanii Princes Dalyla akitoa burudani kwa wadau wa Jukwaa la Sanaa la BASATA mapema wiki hii
Sehemu wa wadau wa Sanaa waliohudhuria Jukwaa la Sanaa wiki hii wakifuatilia kwa makini burudani.
NEWS RELEASE
MSANII
mahiri wa muziki wa kizazi kipya Mwasiti Almas amewataka wasanii
wenzake kuwa wabunifu katika kutanua mianya ya kujiingizia kipato na
kuhakikisha wanazingatia maadili wawapo jukwaani ili kulinda hadhi zao.
Mwasiti
ameyasema hayo mapema wiki hii wakati akijibu maswali ya wadau wa
Jukwaa la Sanaa linalofanyika kwa mwezi mara mbili ziku za Jumatatu
makao ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Ilala Sharif Shamba.
Wadau
hao wa Sanaa walitaka kujua ni kwa nini wasanii wengi hufilisika mara
wanaposimama kufanya shughuli za Sanaa na wengine wamekosa ubunifu
wawapo kwenye maonesho au wanapozalisha kazi zao hali ambayo inawafanya
watumie sehemu za siri za miili yao katika kutafuta mvuto kwa mashabiki.
“Wasanii
wengi wanang’ang’ania kwenye sanaa pekee. Hawawekezi kwenye miradi
mingine. Kuwa na umaarufu si kuwa na fedha bali umaarufu ni njia tu
inayokusaidia kuingia kwenye sekta na miradi mbalimbali kwa ajili ya
kujiimarisha kimapato” alisema Mwasiti wakati akifafanua suala la
wasanii kufilisika mara wanapochuja kwenye Sanaa.
Alizidi
kueleza kwamba wasanii waliopo sasa hawana budi kutambua kwamba
hawatakuwepo muda wote bali kuna leo na kesho hivyo lazima kuiandaa
kesho sasa.
“Umri
wa wasanii unaenda, waliopo sasa hawawezi kuwepo kesho kwani kuna
wasanii wengi wanaibuka na lazima wapate nafasi. Ni muhimu sana kwa
wasanii kuliona hili. Huko nyuma kaka na dada zetu walipata shida
ilikuwa ngumu lakini kwa sasa wasanii tunapata kipato na baadhi
wanajitahidi kuwekeza” alisema Mwasiti.
Kuhusu
wasanii kufanya maonesho yasiyo na maadili, Mwasiti alisema kwamba
inasikitisha sana kwani katika hali ya kawaida msanii anayejitambua na
kuthamini utu na hadhi yake hawezi akafanya maonesho ya uchi kwani
matendo ya wasanii huathiri sana jamii inayowazunguka.
“Matendo
yetu wasanii huathiri sana jamii inayotuzunguka. Sisi ni binadamu na
tuna leo na kesho. Sipendi siku zijazo watoto wetu waje kuuliza na
kushangaa yale tuyafanyayo sasa maana yataendelea kuonekana” alisema
Mwasiti.
Katika
Jukwaa hilo BASATA lilimwalika Mwasiti na wa msanii mwenzake wa kike
Princes Dalyna anayefanya muziki wa reggae ili kueleza historia,
changamoto na mafanikio waliyoyapata katika kazi zao za Sanaa.
Post a Comment