Na Hillary Shoo, Singida
MGOMBEA
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha
Ukombozi wa Umma (CHAUMA) Hashim Rungwe, amesema akichaguliwa kuwa Rais
atajenga vituo maalumu vya walemavu wa ngozi Albino pamoja na wazee ili
waishi kwa amani na utulivu.
Rungwe
aliyasema hayo jana wakati akizungumza kwenye mkutano wa kampeni wa
chama chake uliofanyika kituo cha zamani cha mabasi, Mjini Singida.
Alisema
lengo la kutengeneza vituo hivyo ni kutokana na walemavu hao kuandamwa
kila mara na watu wasiowatakia mema na kuwavizia kila kona ili waweze
kuwakata viungo vyao kutokana na imani potofu.
“
Hawa mimi nitawajengea vituo maalum na watakaa huko kwa maisha yao
ikiwa ni pamoja na kuwapatia elimu bora ili na wao wajione kuwa wako
katika nchi ya amani na utulivu, pia wazee tutawatunza kwa kufanya kazi
sisi,wako wasiojiweza nao pia nitafanya hivyo hivyo, sawa jamani. “
Alisema Rugwe na kuamsha nderemo na vifijo.
Aidha
alisema mbali na kujenga vituo hivyo pia serikali atakayounda haitakuwa
na msururu wa mawaziri kwani kufanya hivyo ni kuwanyima watu wengine
fursa za uongozi ndani ya nchi hii.
Pia
alisema endapo atachaguliwa kuwa Rais atahakikisha kuwa magari
yatakayotumika kwa viongozi ni yale aina ya Landrover Defender ambayo
gharama zake sio kubwa kama ilivyo kwa mashangingi ambayo yanauzwa bei
ghali wakati wananchi wanataabika na njaa.
“
Njaa ni mbaya jamani , kila kona ni njaa tu, hii kitu kwangu
haitakuwepo kila mtu afanye kazi sio kulia lia njaa, njaa, njaa wakati
nguvu tunazo za kuweza kufanya kazi, kila mtu afanye kazi.”Alisisitiza
Rungwe huku akishangiliwa kutokana na staili yake ya kuhutubia kwa
mbwembwe.
Katika
hatua nyingine Mgombea huyo alisema Serikali yake itanunua ndege aina
ya helpkopta kwa ajili ya kumwagilia mashamba ya wakulima mara tatu kwa
wiki lengo ni kuhakikisha uzalishaji wa mazao ya chakula unapatikana
wakati wote bila kutegemea mvua.
“Hili
linawezekana tuna maziwa na mito mingi hivyo hakuna sababu ya wakulima
kutegemea mvua, ndege zitafanya kazi ya kumwagilia mashamba yenu, na
hili ni jambo linalowezekana, nimetembea nchi nyingi za Saudi Arabia na
kiarabu zinatumia utaratibu huu.” Alisema Rungwe na kushangiliwa.
Aidha
alisema ni wakati sasa wa CCM kupumzishwa kwani hawana jipya na kuwa
wamechoka na sera zilezile kuwa watawaletea maendeleo kwani miaka 50
sasa bado Watanzania wana hali mbaya na kila kona utasikia njaa mbaya
njaa mbaya.
“Tuwapumzishe
hawa wamechoka , wanatuita malofa na wapumbavu sasa ni wakati wa malofa
na wapumbavu kuongoza nchi hii, uwezo wao wa kuongoza ni mdogo, betri
hazina chaji wapuuzeni hawa, mimi betri ina chaji imejaa full, nipeni
miaka mitano muone kazi yangu.” Alisema.
Post a Comment