Serikali imesema bei ya umeme nchini inatarajiwa kushuka kwa kiwango kikubwa baada ya kuanza uzalishaji wa nishati hiyo kwa kutumia gesi asilia kutoka Mtwara hadi Kinyerezi, Dar es Salaam.
Waziri
wa Nishati na Madini, George Simbachawene alisema hayo, Dar es Salaam,
jana wakati akikagua mradi wa bomba la gesi na kuwashwa kwa mitambo ya
kuzalisha umeme ya Ubungo II na Kinyerezi I.
“Jambo
hili ni kubwa na la kihistoria kwa nchi hii kwa kitendo cha kuanza
kutumia umeme wa gesi, tulipaswa kusimama hata kwa dakika tatu
kusherehekea mafanikio haya kupitia mradi kubwa wa serikali uliogharimu
dola za Marekani 1.22 bilioni,” alisema Simbachawene.
Alisema
mitambo ambayo itawashwa kwa kutumia umeme wa gesi ni Ubungo II,
Kinyerezi I na Tegeta ambayo kwa ujumla ndiyo itasaidia kutatua tatizo
la mgao wa umeme kwa sababu awali ilikuwa haifanyi kazi kwa kukosa gesi.
“Kwa
kiasi kikubwa mradi huu wa kufua umeme kwa gesi umekamilika nchini na
ndani ya mwezi Septemba na Oktoba, mwaka huu, mitambo yote yenye uwezo
wa kuzalisha megawati 335 itakuwa imewashwa na hivyo kuondoa tatizo la
umeme hapa nchini, ”alisema Simbachawene na kuongeza:
“Juzi
(Septemba 17) tuliwasha umeme wa jumla ya megawati 90 kutoka katika
mitambo ya Tanesco ya kuzalisha umeme wa gesi ya Symbion na Ubungo II
yenye urefu wa futi za ujazo wa bomba 20milioni na zoezi hili
linaendelea hadi Oktoba 20, mwaka huu”.
Simbachawene alisema hilo litakuwa limekamilika kwa kuzalisha megawati 335 na nchi kuingia katika uchumi wa kati.
Post a Comment