Rais wa
Burkina Faso Michael Kafondo amenyang’anywa madaraka ya kuendelea
kuiongoza nchi hiyo baada ya kuondolewa madarakani kwa kiongozi wa Taifa
hilo Blaise Compaore.Hatua hiyo imekuja baada ya viongozi hao wawili wa
Serikali Kafondo pamoja na Waziri Mkuu wake Isaac Zida kuzuiliwa
kuingia kwenye mkutano wa Mawaziri na walinzi waliokuwa wa Rais Compare.
Vurugu
zilitanda katika mji mkuu wa nchini hiyo Ouagadougou huku risasi
zikirushwa hovyo hewani ili kuwatawanya waandamanaji waliojitokeza kwa
wingi kupinga rais huyo kuendelea kubaki madarakani.
Shirika
la Voice of America limesema Rais huyo, Waziri mkuu pamoja na viongozi
wengine wa Serikali waliwekwa chini ya ulinzi na kikosi cha usalama RSP
kinachomsapoti Rais aliyeondoka madarakani Blaise Compaore.
Compaore
aliondolewa madarakani kwa nguvu ya wananchi Octoba 2014 na kuteuliwa
Rais wa mpito kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu October 11 mwaka huu.
Post a Comment