Staa wa filamu ya Chausiku, Shamsa Ford amesema hatobadilisha msimamo wake wa kushabikia vyama vya upinzani kwa kulaghaiwa na wasanii wachache kwa maslahi yao binafsi .
Shamsa amesema hayupo tayari kufuata maamuzi ya watu wengine hata kwa lundo la fedha kwani kufanya hivyo ni kujidhalilisha .
“Mimi
nitabaki huku kwa kuwa nahitaji mabadiliko,kila siku wasanii tunalia
tukidai tunaibiwa na hakuna utekelezaji na matokeo yake tunapewa ahadi
zisizoisha.”Amesema Shamsa
Aidha , Shamsa Ford aliwataka mashabiki kuwaona kama watu wakawaida kwani baada ya siasa maisha yataendelea kama zamani.
Post a Comment