KAULI ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Bulembo kwamba “CCM haitafanya makosa kukabidhi Ikulu kwa wapinzani” imezua mjadala.
Bulembo alitoa kauli hiyo kwenye mkutano wa kampeni za urais wa mgombea wa chama chake Dk. John Magufuli Kigoma.
“Serikali
imefanya makosa mengi na Chama Cha Mapinduzi kimefanya makosa mengi
lakini hakitofanya kosa la kuruhusu chama pinzani kuingia Ikulu,” alisema Bulembo.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana kwenye Ngome ya UKAWA, Jijini Dar es
Salaam, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alimtaka Mwenyekiti wa Tume
ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva kukemea kauli hiyo.
Pamoja
na hivyo Mbowe aliitaka CCM kufuta kauli kwa kuwa ni ya uchochezi
ambayo inatoa tafisiri ya kutokuwepo umuhimu wa kufanya uchaguzi.
Mbowe
alisema kuwa, tangu kutolewa kwa kauli hiyo, hakuna hatua yoyote
iliyochukuliwa na NEC wala kiongozi yoyote wa CCM aliyekemea au
kuzungumzia na kuwa “inaonekana ni mipango ya chama hicho.”
Alisema kuwa, kauli hiyo ingetolewa na chama pinzani NEC isingevumilia na ingechukua hatua haraka.
Hata hivyo alisema CCM inalindwa na sheria mbovu na kandamizi na kuwa, zinahitajika kuondolewa.
Alifafanua kuwa, mfano wa sheria hiyo ni kutangazwa kwa matokeo ya urais ambapo kwa mujibu wa sheria hayapingwi mahakamani.
Msikilize Mbowe akiongea hapo chini
Msikilize Mbowe akiongea hapo chini
Post a Comment