Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WANANCHI WAMTANGAZA JAFARI MNEKE NDIYE MBUNGE MBELE YA LOWASSA..WAMWAMBIA WENGINE TUPA KULE

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Masasi, Mkoani Mtwara, waliofikia kusikiliza sera zake katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Boma, leo Septemba 22, 2015. Ambapo amewashukuru wananchi wa Mji wa Masasi kwa mapokezi makubwa waliyompatia.
Na Mwandishi Wetu
Mgombea ubunge jimbo la Newala Vijijini kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF) anayeungwa mkono na Muungano wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Bw. Jaffar Mneke amemweleza mgombea Urais wa muungano huo Bw. Edward Lowassa kuwa wananchi wa jimbo hilo na mikoa ya Kusini kwa ujumla wanajambno lao zito; kujengewa Newala na Kusini mpya itakayofaidika kutokana na raslimali mbalimbali ikiwemo gesi.
Bw. Mneke aliyasema hayo juzi (Jumatatu) alipopewa nafasi ya kueleza kero za wananchi wa jimbo hilo katika mkutano uliohutubiwa na Bw. Lowassa ambapo aligusia kero za maji, bei ndogo ya zao la korosho na ahadi hewa walizopewa wananchi za kujengewa barabara.
“Katika suala la maji licha ya Newala kuwa na vyanzo vingi na vikubwa vya maji kama vile Mitema, Mkunya Makundeko, Chemchem za Ndanda pamoja na Mto Ruvuma lakini ni maajabu kuwa leo miaka 50 ya Uhuru wananchi hawana maji safi na salama,” alisema.
Alitumia dakika tano alizopewa pia kuanisha tatizo la bei ya korosho; zao muhimu la kiuchumi katika Mikoa ya Kusini. “Kukosekana soko la uhakika la Korosho ni matokeo ya sera mbovu za CCM zilizoshindwa kuweka fursa bali urasimu wa upatikanaji wa pembejeo na mfumo mbovu wa Stakabadhi ghalani.
“Kupitia mfumo huo mbovu serikali imekuwa ikiwakopa wakulima na mpaka muda huu kuna wakulima wengi hawajalipwa pesa za miaka mitatu iliyopita. Hali hii kamwe haiwezi kuhamasisha watu kushiriki katika kilimo,” alisema Mneke na kushangiliwa.
Kuhusu barabara alisema licha ya Serikali kuahidi kujenga barabara ya Newala-Mtwara na Newala-Mtama lakini walichokishuhudia wananchi ni kupewa ahadi hewa ambao haikutekelezwa kwa zaidi ya miaka 10 sasa.
Kabla ya Lowassa kueleza atakavyotatua kero hizo, mratibu wa ikampeni za Ukawa, Bw. John Mrema (Chadema) alimaliza utata kuhusu wagombea wanaopaswa kusimama kwa niaba ya muungano huo katika majimbo ya Newala Vijijini na Mjini. Wagombea wa vyama vya CUF na Chadema wote walikuwa wamechukua fomu na kuzua taharuki kwa wafuasi wao.
“Natangaza rasmi kuwa Bw. Mneke na Manguya Wote kutoka CUF ndio tulioamua wawakilishe Ukawa katika majimbo ya Newala Vijijini na Mjini. Nawaomba makamanda wa Chadema waheshimu uamuzi huu na wajitoe ili kuwaunga mjkono wenzetu hawa la sivyo tutachukua hatua za kinidhamu,” alisema Mrema ambaye aliwaambnia wagombea wa Chadema kuwa hata yeye amelazimika kuliacha jimbo la Vunjo kumwachia James Mbatia wa NCCR-Mageuzi.
Akiwanadi Bw. Mneke (PICHANI) na Manguya, Lowassa alisema amezisikia kero hizo kutoka kwa wawakilishi hao wa wananchi na kuwapa wananchi changamoto ya kuhakikisha wanawapigia ili atengeneze nao timu ya kupeleka maendeleo ya haraka Newala na Kusini kwa ujumla ambapo wananchi walipiga mayowe kuwatangaza wagombea hao kuwa ndio wabunge wao.
Katika mkutano huo Lowassa aliendelea kusisitizia kuwa atawasaidia vijana na akina mama hasa wamachinga, bodaboda na Mamantilie ili kugeuza changamoto zao za sasa kuwa fursa za kujiajiri na kujikwamua kiuchumi.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top