Baadhi
ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi wa Jimbo la Chake chake Pemba
wakifuatilia hotuba na Mke wa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mama
Asha Suleiman hayupo pichani wakati akizungumza nao kwenye ukumbi wa
Hoteli ya Hifadhi Chake chake Pemba.
Mke
wa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mama Asha Suleiman akibadilishana
mawazo na Vijana wa CCM Jimbo la Chake chake katika Kikao cha kutafakari
zoezi zima la Kampeni na kuelekea kwenye uchaguzi Mkuu.
Mjumbe
wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi Balozi
Seif Ali Iddi akizungumza na Vijana wa CCM Jimbo la Chake chake kwenye
Ukumbi wa Hoteli ya Hifadhi Chake chake Pemba.
Balozi
Seif Ali Iddi akipokea baadhi ya Kadi za Wanachama wa Chama cha
Wananchi { CUF } walioamua kukihama Chama hicho na kujiunga na Chama cha
Mapinduzi hapo Hifadhi Hoteli Chake chake Pemba.
Baadhi
ya Vijana wa CCM wakifuatilia hotuba ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM,
Taifa Balozi Seif hayupo pichani wakati akizungumza nao hapo Hifadhi
Hoteli Chake chake Pemba.
Picha na – OMPR – ZNZ
Mjumbe
wa Kamati Kuu ya Halmshauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi Balozi
Seif Ali Iddi amewanasihi Wananchi hasa Vijana wa Majimbo la Kisiwa cha
Pemba kubadilika kwa lengo la kuachana na tabia ya kufanywa ngazi na
baadhi ya Watu wakati wa uchaguzi na baadae kuamua kujinufaisha wao
binafsi na familia zao.
Alisema
miaka isiyopunguwa ishirini wananchi hao wamekuwa wakitumiwa kama
vitega uchumi na watu ambao wamekuwa na hulka ya kuwakimbia mara tu
baada ya kuwachagua.
Balozi
Seif Ali Iddi alitoa nasaha hizo wakati akizungumza na Vijana wa Chama
cha Mapinduzi wa Jimbo la Chake chake wakiwemo pia wale Vijana
walioamua kuacha chama cha Wananchi { CUF } na kujiunga na CCM Mkutano
uliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Hifadhi Tibirinzi Chake Chake
Pemba.
Post a Comment