Mgombea
Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif
Sharif Hamad, akiwahutubia wafuasi wa Chama hicho katika viwanja vya
Fumba Kids, jimbo la Dimani.
Mgombea
Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif
Sharif Hamad, akimtambulisha mgombea Uwakilishi wa jimbo la Dimani
kupitia chama hicho Bw. Mohamed Hashim Ismail, katika mkutano
uliofanyika viwanja vya Fumba Kids.
Wafuasi wa CUF wakifuatilia hotuba na mgombea urais wa Chama hicho katika viwanja vya Fumba Kids, jimbo la Dimani.
Afisa
uchaguzi wa CUF Bw. Muhene Said Rashid, akitoa elimu ya wapiga kura kwa
wafuasi wa chama hicho kwenye mkutano uliofanyika viwanja vya Fumba
Kids, jimbo la Dimani.
Mgombea
Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif
Sharif Hamad, akiungana na wafuasi wa CUF kuimba nyimbo za kuhamasisha
alipowasili katika barza ya “Radio One” kuonana na wanabarza hiyo.
(Picha na Salmin Said, OMKR)
MKOA WA MJINI MAGHARIBI
Na: Hassan Hamad, OMKR
Mgombea
Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif
Sharif Hamad, amesema iwapo atachaguliwa kura Rais atazipitia upya
fidia walizolipwa wananchi wa maeneo ya Fumba, Bwefumu na Bweleo ili
kuwalipa fidia zinazostahiki kulingana na maeneo yao yaliyochukuliwa kwa
ajili na uendelezaji wa maeneo huru ya kiuchumi.
Amesema
serikali atakayoiongoza iwapo atachaguliwa kuwa Rais inakusudia
kuondosha kabisa vitendo vya dhulma dhidi ya wananchi, hivyo wananchi
hao watapatiwa fidia zinazostahiki baada ya kufanyiwa tathmini.
Akizungumza
katika mkutano wa kampeni za chama hicho uliofanyika viwanja vya Fumba
jimbo la Dimani, Maalim Seif amesema Serikali inapaswa kulipa fidia
zinazoendana na thamani ya maeneo ya wananchi inapoamua kuyachukua kwa
maslahi ya umma, na kwamba serikali yake haitosita kufanya hivyo katika
maeneo ya ukanda wa Fumba.
Aidha
Maalim Seif amewahakikishia wananchi wa maeneo hayo upatikanaji wa maji
safi na salama, ili kuondosha kabisa tatizo hilo linalowakabili kwa
muda mrefu sasa.
Akizungumzia
kuhusu mchakato wa uchaguzi Maalim Seif amesema licha na vitendo
vinavyofanywa kuashiria kuingilia kati mchakato huo, uchaguzi mkuu
utafanyika tarehe 25 Oktoba kama ulivyopangwa.
Kabla
ya mkutano huo Maalim Seif alifanya ziara ya kutembelea baadhi ya
matawi na barza za majimbo ya Kijitoupele, Dimani Mwanakwerekwe na
Welezo ikiwemo barza ya “Radio One” na kuelezea kuridhishwa na jinsi
wananchi walivyohamasika kushiriki uchaguzi ujao.
Nae
Mgombea Uwakilishi wa jimbo la Dimani kupitia chama hicho Bw. Mohamed
Hashim Ismail amewataka wananchi wanaoitakia mema Zanzibar kuwachagua
wagombea waliosimamisha na Chama Cha Wananchi CUF katika uchaguzi ujao
ambao amesema ni muhimu kwa ukombozi wa Zanzibar.
Amesema
akiwa mgombea wa jimbo hilo atahakikisha kuwa anapita nyumba kwa nyumba
ili kuona kuwa kila aliyejiandikisha kupiga kura wakiwemo wagonjwa
wanatekeleza jukumu hilo.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Timu ya ushindi CUF Mhe.
Ismail Jussa Ladhu amelishauri jeshi la polisi kuendeleza mahumiano
mema kati yake na wananchi kama lilivyofanya wakati wa kuanza kwa
kampeni.
Amesema
ni vyema kwa jeshi hilo kufanya juhudi za kudhibiti vitendo
vinavyoashiria shari ikiwa ni pamoja na baadhi ya hujuma vinazofanywa
dhidi ya majengo na wanachama wa chama hicho.
Post a Comment