KAMPENI
za wagombea Ubunge jimbo la Arusha Mjini zimesimama kufuatia kifo cha
Mgombea Ubunge wa chama cha ACT-Wazalendo, Estomiah Mallah aliyefariki
usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya KCMC iliyopo wilaya ya Moshi,
Kilimanjaro, baada ya kuugua ghafla ugonjwa wa shinikizo la damu.
Akithibitisha
kupokea taarifa za kifo cha Mgombea huyo Mkurugenzi wa Jiji la Arusha,
Juma Idd ambaye pia ni Msimamizi mkuu wa Uchaguzi katika jimbo hilo, Idd
amesema kuwa kampeni ambazo zitaendelea ni za urais na udiwani, lakini
wabunge mpaka tume ya uchaguzi ipange upya ratiba.
“Kweli
mgombea amefariki na nimepata taarifa za kifo hiki leo saa 12:00
asubuhi, toka kwa katibu wa chama chake marehemu ACT-Wazalendo, Eliamam
Motivo,” amesema.
Aidha ametoa pole kwa wafuasi wa chama hicho kwa kuondokewa na mpendwa wao na wapo pamoja katika kipindi hiki kigumu.
Katibu
wa Jimbo la Arusha wa Chama cha ACT-Wazalendo, Eliamam Motivo amesema
amepokea kwa masikitiko makubwa msiba wa mgombea wao na Mshauri Mkuu wa
Chama chao kwa mkoa wa Arusha.
“Mzee
alikuwa haumwi lakini kwenye mkutano wa mgombea urais wa chama chetu
Oktoba 6, alipanda jukwaani na baada yakushuka alisema hajisikii vizuri
na kesho yake ambayo Oktoba 7 alikwenda hospitali ya St. Thomas na
alipatiwa matibabu ila hali yake iliendelea kuwa mbaya na tuliamua
kumwamishia hospitali ya KCMC na usiku wa kuamkia leo saa saba
usiku alifariki,” amesema.
Motivo alisema chama hicho kimesimamisha kampeni zote, kwa siku tatu ili kuomboleza msiba huo.
Post a Comment