Aliyekuwa kada mkongwe wa CCM, mzee Kingunge Ngombale Mwiru amekishukia chama chake hicho cha zamani na viongozi wake wa sasa kwa madai kuwa ‘kimechanganyikiwa’.
Akiongea
leo katika mkutano wa kufunga kampeni za vyama vya upinzani vinavyounda
Ukawa baada ya kumnadi mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa, Mzee
Kingunge alidai kuwa mwenendo wa kampeni na matamko ya viongozi wa ngazi
za juu wa chama hicho huku akitoa mfano wa lugha kali pamoja na matusi
yaliyotumika kwenye majukwaa ya kampeni.
Mzee
Kingunge alimsihi Rais Jakaya Kikwete kutotumia nguvu ya dola kuzuia
sauti ya wananchi walio wengi ambao alidai wameamua kumuingiza Ikulu
Edward Lowassa.
Alimshauri Rais Kikwete kujipanga kukabidhi kwa amani madaraka kwa mgombea urais atakayeshinda ambaye anaamini ni Lowassa kama alivyokabidhiwa nafasi hiyo kutoka kwa rais wa serikali ya awamu ya tatu, Benjamin Mkapa.
Alimshauri Rais Kikwete kujipanga kukabidhi kwa amani madaraka kwa mgombea urais atakayeshinda ambaye anaamini ni Lowassa kama alivyokabidhiwa nafasi hiyo kutoka kwa rais wa serikali ya awamu ya tatu, Benjamin Mkapa.
“CCM
imekuwa na utaratibu wa kukabidhi madaraka kwa amani, Mwinyi
alimkabidhi madaraka Mkapa kwa amani, Mkapa naye alimkabidhi yeye kwa
amani, sasa nay eye afanye hivyo.”
Alisema
kuwa kuna dalili kwamba Rais Kikwete anataka kuyapinga matakwa ya
wananchi walio wengi kwa kuchakachua matokeo na kufanya hujuma kwenye
mchakato wa uchaguzi kwa kutumia nguvu ya dola hivyo akamsihi aache kwa
kuwa ataliingiza taifa kwenye machafuko.
Mwanasiasa
huyo mkongwe alionesha kusikitishwa na kauli zilizotolewa na Rais
Kikwete kwa kuwachukulia wapinzani kama ‘adui’ na kwamba wapigwe.
Alisema mchezo wa siasa ni ushindani na sio uadui.
Mzee
Kingunge aliwakumbusha wananchi kuwa mwalimu Nyerere aliwahi kumtangaza
adui wa Tanzania anayefaa kupigwa kuwa ni Idd Amin na sio wananchi wa
Tanzania.
“Nyerere alikaa na wazee wa Dar es Salaam, akasema tumpige adui Idd Amin, akatangaza apigwe na kweli tukampiga,” alisema na kudai kuwa alishangaa kumsikia Rais Kikwete akitangaza kuwa wapinzania ni maadui na wapigwe.
Mzee
Kingunge alitangaza kuitosa CCM na kuhamia upande wa Mabadiliko akidai
kuwa viongozi wa sasa wa CCM wamepoteza dira na chama hicho kimekosa
muelekeo na kimekata pumzi, hivyo hakiwezi tena kuwafikisha watanzania
kwenye kilele cha mafanikio.
Post a Comment