Ligi
kuu ya Vodacom Tanzania (VPL) inatarajiwa kuendelea kesho Jumatano kwa
michezo minne kuchezwa katika viwanja tofauti nchini, huku timu 8
zikisaka kupata pointi tatu muhimu.
Uwanja
wa Taifa jijini Dar es salaam Young Africans watawakaribisha Toto
Africans, mchezo utakaonza majira ya saa 10:30 jioni, mjini Shinyanga
Stand United watakua wenyeji wa Majimaji katika uwanja wa Kambarage
mjini humo.
Tanzania
Prisons watawakaribisha Simba SC katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya,
huku Wagosi wa Kaya, Coastal Union wakiwakaribisha Kagera Sugar katika
uwanja wa Mkwakani jijini Tanga.
Alhamis
ligi hiyo itanendelea kwa michezo minne pia kucheza katika viwanja
mbalimbali, JKT Ruvu wataikaribisha Mtibwa Sugar uwanaj wa Karume jijini
Dar es salaam, Mwadui FC watacheza dhidi ya Mgambo Shooting katika
uwanja wa Mwadui Complex mjini Shinyanga.
Jijini
Mbeya, Mbeya City watawakaribisha African Sports katika uwanja wa
Sokoine, huku Ndanda FC wakiwa wenyeji wa waoka mikate wa bakhresa Azam
FC katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
Post a Comment