Mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa amesema amejiandaa na yupo tayari kuwaongoza Watanzania akiwa rais wa awamu ya tano.
Akizungumza kwenye Uwanja wa Ruanda Nzovwe- Mbeya Mjini, Lowassa alisema: “Ninatosha, nitumeni kwa kura zenu… nipeni kura za kutosha niwatumikie.”
Lowassa ambaye alisema anasikia deko kutokana na wingi wa watu, alisema misamaha ya kodi kwa sasa ni Sh1.6 trilioni na kwamba atahitaji Sh1.3 trilioni kati ya hizo kwa ajili ya elimu itakayolipiwa na serikali kuanzia chekechea hadi chuo kikuu.
Pia, aliendelea kuwasisitizia wananchi, umuhimu wa kulinda kura zao baada ya kupiga hadi kitakapoeleweka.
“Wana
Mbeya, kuna rafiki yangu aliniambia umeshinda, mwingine akasema huwezi
kushinda kwa sababu wataiba kura. Mimi nasema nipeni kura nyingi hata
wakiiba zitoshe, kaeni kituoni mpaka kieleweke, huu ni mwaka wa kuitoa
CCM madarakani,” alisema Lowassa.
Lowassa
aliueleza umma huo, kwamba kuna watu wanapita mitaani kutoa rushwa na
kununua shahada za kura, lakini wasiwe na hofu nao.
“Wakikupa
hizo hela, kula, akikupa laki tano, mwambie akupe milioni moja,
akishakupa na akaendelea kukusumbua, mwambie asikusumbue hizo ni pesa za
Lowassa.
Post a Comment