Mshambuliaji wa timu ya Stand United ya Shinyanga, Elias Maguli.
Na Said Ally
AKIWA ndiye kinara mpaka sasa kwenye orodha ya wafungaji ligi kuu baada ya kufunga mabao nane, mshambuliaji wa timu ya Stand United ya Shinyanga, Elias Maguli, ameorodheshwa akiwa miongoni mwa wachezaji wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’ ambao wanatarajia kucheza na timu ya Algeria.
AKIWA ndiye kinara mpaka sasa kwenye orodha ya wafungaji ligi kuu baada ya kufunga mabao nane, mshambuliaji wa timu ya Stand United ya Shinyanga, Elias Maguli, ameorodheshwa akiwa miongoni mwa wachezaji wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’ ambao wanatarajia kucheza na timu ya Algeria.
Stars itavaana na Algeria kwenye mchezo wa kutafuta tiketi ya kucheza Kombe la Dunia mwaka 2018 ambalo litafanyika nchini Urusi.
Maguli ameorodheshwa katika kikosi cha wachezaji 28 wa Stars, ambao
wataenda nchini Oman kwa ajili ya kuweka kambi ya siku 11 kabla ya
kurejea nchini Novemba 11 kujiandaa na mchezo wake dhidi ya Algeria,
ambao utapigwa jijini hapa Novemba 14.
Akizungumza na Championi Jumatano, Kocha Mkuu wa Stars, Boniface
Mkwasa, alisema kuwa ameamua kumwita mshambuliaji huyo pamoja na
wachezaji wengine kwa ajili ya kuja kukiongezea nguvu kikosi chake
kuhakikisha kinafanya vyema na kuiondoa timu hiyo.
“Kikosi chetu ambacho kitaingia kambini Novemba 1, hakitakuwa na
mabadiliko sana kutokana na wachezaji waliokuwepo kuonyesha kuanza
kuzoeana lakini ndani yake tumeamua kuwaongeza wachezaji wapya kwa ajili
ya kuingiza nguvu mpya ndani ya timu hiyo.
“Mmoja wa wachezaji hao ni mshambuliaji wa Stand, Elias Maguli ambaye
amepata nafasi ya kuingia baada ya kuonyesha kiwango cha hali ya juu
katika michezo ya ligi pamoja na kuisaidia timu yake,” alisema Mkwasa.
Wachezaji wengine wapya waliojumuishwa katika kikosi hicho ni pamoja
na Malimi Busungu (Yanga), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Ramadhan Kessy
na Jonas Mkude (Simba), Salum Aboubakar ‘Sure Boy’ (Azam), huku Deus
Kaseke (Yanga) na Rashid Mandawa (Mwadui) wakitemwa.
Post a Comment