MGOMBEA
Ubunge jimbo la Iringa Mjini kupitia Chadema, Mchungaji Peter Msigwa na
wenzake watatu, wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Iringa
wakituhumiwa kushambulia na kujeruhi askari polisi wawili.
Katika
mashitaka hayo, Msigwa ambaye alikuwa Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini
na Waziri kivuli katika Wizara ya Maliasili na Utalii katika bunge
lililopita, alifikishwa na wenzake watatu shitaka linalowakabili
washitakiwa 10 kwa makosa hayo.
Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Blandina Manyanda aliwataja washitakiwa wengine waliofikishwa mahakamani hapo mbele ya Hakimu Makazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Iringa, David Ngunyale, kuwa ni Edwine Sambala(66), Joseph Mgima (56) na Josephat Chengula (36).

Manyanda
alisema kuwa washitakiwa hao walitenda makosa hayo Septemba 28 mwaka
huu, ambapo watuhumiwa hao kwa pamoja walifanya makosa hayo kwa kufanya
kosa la uvunjifu wa amani katika eneo Sambala Kata ya Gangilonga na
kuwasababishia usumbufu kwa watumiaji wa barabara ya Iringa Dodoma.
Post a Comment