Mgombea
ubunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia chama cha APPT– Maendeleo,
Elisiana Tabwe, amewataka Watanzania wasipoteze bahati ya kutomchagua
mgombea urais kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward
Lowassa, kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Tabwe
alimmwagia sifa Lowassa kupitia Chadema juzi wakati wa mdahalo wa
wagombea ubunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini uliofanyika Ngokolo na
kuandaliwa na Radio Faraja mjini humo kuwa Lowassa ndiye Rais anayefaa
kuongoza nchi.
“Ndugu
zangu, najua mtanishangaa, lakini bila kumung’unya maneno wala
kushinikizwa na yeyote, nawaombeni katika uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka
huu, mkamchague mgombea urais Lowassa, kiongozi ambaye mnatambua
utendaji wake wa kazi,” alisisitiza Tabwe. Hata hivyo, mgombea ubunge wa
Chadema katika Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi, na mgombea
wa CCM, Steven Masele, walikacha mdahalo huo.
Post a Comment