Siku moja baada ya kutangaza kujitoa CCM, kada mkongwe wa chama hicho, Balozi Juma Mwapachu amesema uamuzi alioufanya ni sahihi ambao hata Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere angekuwa hai angeufanya kwa sasa.
Balozi
Mwapachu alieleza hayo jana katika mahojiano maalumu na kuongeza kuwa
chama chake cha zamani kimepoteza mwelekeo kwa kuwa kinara wa kuvunja
katiba na taratibu kitendo ambacho Nyerere alikichukia katika maisha
yake.
Alisema
anafahamu fika kuna watu watakosoa uamuzi wake huo lakini hatababaishwa
na maneno yao na atasimamia msimamo wake huo huku akieleza kuwa
anajisikia amani kujitoa katika siku ya kumbukumbu ya miaka 16 ya kifo
cha Nyerere.
Mwapachu
alitangaza kujitoa CCM juzi akisema kilivunja taratibu wakati wa
mchakato wa uteuzi wa mgombea wa urais uliofanyika Julai ambao Dk John
Magufuli alichaguliwa.
“Nimefanya
makusudi kujitoa wakati huu kwa sababu hata Nyerere mwenye angekuwapo
hai leo hii angefanya uamuzi kama niliofanya. Hata yeye alikuwa
ameshachoshwa na chama chake kwa uvunjaji wa kanuni, taratibu na katiba
na alikwishaona kuwa kinaanza kupitwa na wakati.”
Alisema mengine yanayojitokeza kwa sasa ndani ya CCM yanaonyesha bayana kuwa chama hicho hakiendi na wakati na kilijisahau na kuendesha mambo kama kipo kwenye mfumo wa chama kimoja wakati ni wa vyama vingi.
Alisema mengine yanayojitokeza kwa sasa ndani ya CCM yanaonyesha bayana kuwa chama hicho hakiendi na wakati na kilijisahau na kuendesha mambo kama kipo kwenye mfumo wa chama kimoja wakati ni wa vyama vingi.
Alisema
CCM ya sasa siyo ile aliyojiunga nayo akiwa chuo kikuu, ndiyo maana
amejitoa kutokana na kutekwa na watu wachache ambao humpiga vita mtu
ambaye si mwenzao.
Post a Comment