Mwenyekiti wa NLD, ambaye ni mwenyekiti mwenza wa vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa, Dkt. Emmanuel Makaidi amefariki leo majira mchana katika hospitali ya Nangao mkoani Lindi.
Taarifa
za uhakika zinaeleza kuwa Dkt. Makaidi ambaye alikuwa mgombea ubunge
katika jimbo la Masasi alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la
damu.
Dkt. Makaidi ni mgombea ubunge wa tano kufariki katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu.
Mpekuzi inatoa pole kwa familia, ndugu na jamaa wa Dkt. Emmanuel Makaidi na taifa kwa ujumla.
Post a Comment