Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Nape Nnauye Apata AJALI Mbaya Ya Gari Akitokea Dar Kwenda Lindi



KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amepata ajali mbaya jana usiku akiwa njiani kuelekea Lindi akitokea jijini Dar es Salaam.

Nape ambaye pia ni mgombea Ubunge wa Jimbo la Mtama, Lindi  alipata ajali hiyo baada ya tairi la mbele la gari aliyokuwa akiendesha aina ya Toyota Land Cruiser kupasuka na kupinduka mara kadhaa katika eneo la Nyangao mkoani Lindi.


Katika gari hilo, Nape alikuwa peke yake na ndiye alikuwa akiendesha gari hilo ambapo amepata majeraha madogo  ila anaendelea vizuri.

Kabla ya ajali hiyo, Nape alikuwa jijini Dar es Salaam ambapo aliungana na mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Pombe Magufuli aliyekuwa na mikutano kadhaa ya kampeni katika jiji la Dar na baada ya shughuli hiyo alikuwa akirejea Lindi kuendelea na kampeni kwenye jimbo lake la Mtama.


Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top