Msimamizi
wa uchaguzi jimbo la Iringa mjini Ahmed Sawa amemtangaza mchungaji
Peter Simon Msigwa kuwa mshindi wa kiti cha ubunge wa jimbo la Iringa
mjini baada ya kuwashinda wapinzani wake kwa kura 43,154 katika jumla ya
kura 76,216 zilizopigwa huku mpinzani wake Fredrick Mwakalebela wa CCM
akipata kura 32406,Chiku Abwao wa ACT Wazalendo aliyepata kura 411.
Matokeo
hayo yametangazwa baada ya msuguano mkali baina ya pande mbili yaani
upande wa chama cha mapinduzi CCM na msimamizi wa uchaguzi jimbo la
Iringa mjini kufuatia kupotea kwa masanduku mawili kutoka katika kituo
cha kupigia kura Ipogolo C ambapo baadae tume iliamua upigaji kura
katika kituo hicho urudiwe kuondoa utata na sintofahamu iliyokuwepo.
blog
hii imezungumza na mchungaji Peter Msigwa ili kujua nini kinafuata mara
baada ya ushindi huo wa kishindo ambao umekipa ushindi chama cha
Chadema kwa kupata viti 14 vya udiwani katika jumla ya kata 18 za
manispaa ya Iringa hivyo kutoa nafasi kwa chama hicho kuunda halmashauri
kwa mara ya kwanza.
Awali
jeshi la polisi mkoani Iringa lililazimika kutumia gesi ya kutoa
machozi na maji ya kuwasha kuwatawanya wafuasi wa chama cha Chadema
waliokuwa wanajikusanya kwenda kusikiliza matokeo ya ubunge lakini baada
ya kutangazwa kwa matokeo hayo kundi kubwa la wafuasi wa Chadema
lilivamia halmashauri hiyo gafla wakishangilia ushindi huo huku baadhi
yao wakielezea furaha yao.
Post a Comment