Polisi jijini Dar es Salaam jana usiku walivamia kituo cha kukusanya matokeo ya nchi nzima cha Chadema kilichopo Kijitonyama na kuwakamata watu wote wanaokiendesha.
Mkuu
wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa chama hicho, Tumaini Makene
alisema tukio hilo lilitokea saa nne usiku wakati vijana hao wakiendelea
kukusanya matokeo hayo.
Alisema
kituo hicho kilichokuwa kikiendeshwa na vijana 800 na wengine maelfu
waliokuwa mikoani wakituma matokeo, kilianza kazi hiyo jana asubuhi
kikilenga kukusanya matokeo yote, kuyajumlisha na kujua mshindi kabla ya
matokeo ya jumla ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
“Kituo
chetu kinafanya kazi ile ile kama inayofanywa na kituo cha CCM
kilichopo maeneo ya Mlimani City, tunashangaa polisi kuwakamata watu
wetu,” alisema Makene.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura alisema kwa sasa polisi
wanafanya operesheni nyingi na watu mbalimbali wanakamatwa, hivyo
asingeweza kujua kama watu hao pia wamekamatwa katika operesheni hiyo.
Post a Comment