Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju ametoa mwongozo wa kisheria kufuatia sintofahamu iliyoibuka kwa baadhi ya watanzania kuhusu sababu zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kutovunjwa kwa baraza la mawaziri hadi muda huu huku zikiwa zimebaki siku tano kufanya uchaguzi mkuu.
Masaju
alieleza kuwa kisheria bado sio muda muafaka wa kuvunja baraza la
mawaziri kwa kuwa waziri hupoteza sifa za kuwa waziri wa serikali ya
Tanzania punde kabla ya rais mpya kupatikana.
“Mara
tu kabla rais mteule hajashika madaraka hayo, ndipo waziri anapoteza
nafasi yake ya kuwa waziri. Kwahiyo sasa hata uchaguzi hatujafanya,” alisema.
Aliongeza kuwa suala la siku chache zilizobaki bado liko kisheria kwa kuwa rais mpya bado hajapatikana.
“Japokuwa
ni siku tano sasa zimebaki, lakini uchaguzi ukishafanyika na rais
akapatikana, mara tu huyu rais mteule hajashika madaraka hayo ndipo
waziri anapoteza sifa ya kuwa waziri,” aliongeza.
Majibu
ya kisheria ya mwanasheria mkuu wa serikali yamekuja wakati ambapo
taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii na vijiweni zikieleza
kuwa huenda kutovunjwa kwa baraza la mawaziri kunacheleweshwa kwakuwa
kuna hofu ya mawaziri wengi kukihama Chama Cha Mapinduzi.
Balozi
Juma Mwapachu alikoleza tetesi hizo wakati alipokuwa akirudisha kadi ya
Chama Cha Mapinduzi katika ofisi za chama hicho zilizoko Mikocheni, Dar
es Salaam baada ya kueleza kuwa uamuzi wake unaungwa mkono na mawaziri
wengi wa serikali ya awamu ya nne.
Post a Comment